SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG
Friday, 3 May 2013
MATOKEO KIDATO CHA NNE-2012 KUPANGWA UPYA
National Examination Council of Tanzania (N.E.C.T.A)
Serikali imetangaza uamuzi wa kupanga upya matokeo ya kidato
cha nne ya 2012. Uamuzi huo umetangazwa mapema leo bungeni na Waziri William
Lukuvi, kwa niaba ya Waziri Mkuu. Uamuzi umetokana na kamati ya waziri mkuu
iliyokuwa inachunguza kuhusu matokeo hayo kubaini kuwa matokeo hayo yalipangwa
kwa utaratibu tofauti na uliokuwa unatumika zamani.
Tetesi za awali zilieleza kwamba matokeo hayo yalipangwa kwa
kuzingatia madaraja haya hapa chini, japo Baraza la Mitihani lilikanusha
baadaye kwa kusema kuwa taarifa hizo hazikuwa za kweli:
A = 80%-100%-
B = 65%-79%-
C = 50%-64%-
D = 35%-49%-
F = 0%-34%-
Tume ya Waziri Mkuu imebaini kutumika kwa madaraja tofauti
na uataratibu wa awali. Hivyo basi, matokeo yaliyotangazwa hayatatumika tena
mpaka yaje yaliyopangwa upya. HakiElimu itatoa taarifa rasmi baadaye kuhusu
uamuzi huu wa serikali.
Kila la kheri.
DIAMOND PLATINUM NDANI YA THE SPORAH TV SHOW UK (2013)
baada ya kupia show kadhaa ndani ya London, UK, Diamond alipata nafasi
ya kufanya mahojiano na kipindi cha TV cha "The Sporah Show"
Subscribe to:
Posts (Atom)