Wabunge watano wa Chadema majuz walitimuliwa bungeni na kuamriwa kukaa nje ya Bunge kwa siku tano kutokana na vurugu zilizotokea ndan ya bunge hili kama wewe ni mfatiliji mzuri wa vipind vya bunge utakua unajua habari hii.
Wabunge hao ni Lissu, Hezekiah Wenje (Nyamagana), Highness Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) Godbless Lema (Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini).
Saturday, 20/04/2013
MAKINDA AKOMAA
Spika wa bunge, Anne Makinda.
Wakati Spika wa Bunge, Anne Makinda, akiamua kuwa
adhabu iliyotolewa na Naibu Spika Job Ndugai ya kuwazuia wabunge sita wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhudhuria vikao vitano vya
Bunge ni halali, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe,
amesema hawatakubali kuongozwa kidikteta.
Wabunge walioadhibiwa na Naibu Spika, Job Ndugai, na majimbo yao
katika mabano ni Tundu Lissu (Singida Magharibi), Joseph Mbilinyi (Mbeya
Mjini), Peter Msigwa (Iringa Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Godbless
Lema (Arusha Mjini) na Ezikiel Wenje (Nyamagana).
Adhabu hiyo ilikuja mara baada ya Lissu kutakiwa kukaa chini
alipotaka kuomba mwongozo wakati Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu
Nchemba, akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais (Utawala Bora).
Hata hivyo, juzi Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe,
aliomba mwongozo kwa Spika Makinda, akitaka kufahamu ni lini wabunge
hao sita waliopewa adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya Bunge
wataruhusiwa kwa sababu kanuni iliyotumika kuwaadhibu haikuwa sahihi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za kambi ya
upinzani jana, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alisema kuwa, “sisi
hatutakubali kuishi maisha ya udikteta ndani na nje ya Bunge.”
Alisema iwapo itatolewa hoja ya uongo ni lazima Mnadhimu wa Kambi
ya Upinzani, Lissu ataendelea kusimama hata mara 100 kuomba mwongozo wa
Spika wa Bunge.
“Wasipofanya uovu bungeni Bunge likaendeshwa kwa haki bila upendeleo sisi hatutasimama na kuomba mwongozo wa Spika,”alisema.
Alisema kufuatia uamuzi wa Spika wa kuhalalisha maamuzi ya Ndugai,
watakutana na Kamati ya uongozi ya chama chake na kutoa uamuzi kuhusiana
na mambo hayo.
“Tutakutana mara baada ya waliosimamishwa kurejea bungeni
kuzungumza maana tutapenda kusikia pia maelezo ya Lissu,” alisema Mbowe.
Alisema pia watawakatia rufaa Spika Makinda na Naibu yake juu ya uamuzi walioutoa.
“Tunajua kuwa haki haitatendeka, lakini ni vyema tukaweka
kumbukumbu za kuwa jambo hili liliwahi kufanyika na tukachukua hatua
hizi,” alisema.
Alisema uamuzi wa Spika haukuzingatia kumpa nafasi ya kujitetea
Lissu na wenzake, jambo ambalo ni kosa kwa Makinda kuridhia adhabu hiyo.
Alisema kwa mujibu wa kanuni 74(3), adhabu hiyo ingepaswa kutolewa
na Kamati ya Haki, Kinga na Maadili kuridhika kuwa mbunge husika
ametenda kosa.
“Huku nikutaka kumlinda Ndugai tu maana wangetumia vifungu vya 74
katika kuamua suala hili na kama Lissu angepatikana na kosa wangeweza
kumpa adhabu kubwa zaidi ya hiyo”.
Kwa mujibu wa kifungu cha 74 (3A na B) “Ikiwa ni kosa lake la
kwanza kamati inaweza kushauri mbunge huyo asihudhurie vikao vya Bunge
visivyozidi 10 au ikiwa ni kosa lake la pili au zaidi mbunge asihudhurie
vikao vya Bunge visivyozidi ishirini”.
Awali akisoma mwongozo, Spika Makinda alisema uamuzi uliofanywa na Naibu Spika Ndugai ni sahihi.
Ndugai aliamuru Lissu atolewe nje kwa kukiuka kanuni ya 60 (12), wakati aking’ang’ania kutoa mwongozo.
Makinda alisema adhabu hiyo ilitokana na kukaidi agizo la kiti la
kumtaka kukaa wakati alipompatia nafasi Mbunge wa Viti Maalum, Suzan
Kiwanga (Chadema).
Alisema wabunge wengine watano walipewa adhabu hiyo kwa kosa la
kuwazuia wapambe wa Bunge kutekeleza agizo la Naibu Spika la kutaka
kumtoa nje Lissu na kusababisha fujo.
“Waheshimiwa wabunge kanuni zetu na hasa ya 2 (2), na kanuni ya
5(1) ya kanuni za Bunge imempa mamlaka Spika kufanya uamuzi pale ambapo
hakuna utaratibu wa kanuni,” alisema na kuongeza:
“Aidha, uamuzi unaofanywa na Spika ambao unaruhusu uendeshaji bora
wa shughuli za Bunge ambao unaleta amani na utulivu bungeni utaingizwa
kwenye kitabu cha maamuzi ili kuongoza mwenendo wa baadaye wa uendeshaji
wa Bunge.”
Spika Makinda alisema kitendo kilichofanywa na wabunge hao kamwe hakiwezi kupuuzwa.
“Kwa kitendo kilichotokea Aprili 17 bungeni, hakiwezi kupuuzwa kwa
kuwa ni kitendo dhahiri cha kudhalilisha mamlaka ya spika na kilikuwa
kitendo cha utovu wa nidhamu wa hali ya juu Watanzania wote
waliushuhudia na wanalaani kilichokuwa kinaendelea ukumbini.”
Alisema mbunge yeyote aliyekuwa anaongoza bunge wakati huo, angeweza kutoa uamuzi huo.
“Ninatumia kanuni ya 5(1) , na kanuni ya 2 (2) ya Bunge inayompa
mamlaka Spika kufanya maamuzi ambapo jambo ama shughuli yoyote
haikuwekewa masharti katika kanuni hizi, uamuzi uliofanywa na mheshimiwa
Job Ndugai Naibu Spika wa kuwatoa nje Mheshimiwa Tundu Lissu…..nakubaki
nje kwa kutohudhuria vikao vya Bunge siku tano ni halali,” alisema na
kuongeza:
“Na sasa utaingizwa katika kitabu cha maamuzi ya spika na mbunge yeyote atakayefanya vitendo hivi apewe adhabu hii,” alisema.
CHANZO:
NIPASHE
Katika kijiji kimoja Kaskazini mwa Tanzania,
ndege aina ya Boeing 747 zinatua kwenye kiwanja binafsi, magari yenye
nambari za usajili za milki za kiarabu, zikiendeshwa katika eneo hilo na
yeyote mwenye simu ya mkononi anapotua hapo hupokea ujumbe ambao
haukutarajiwa:
''Hujambo mgeni na karibu UAE.''
Kwa karne nyingi, (Savanna) katika eneo la Arusha lilikuwa makao kwa watu wa jamii ya wamaasai lakini siku hizi mtu sasa anaweza kudhania yuko Dubai moja ya nchi za milki za kiarabu.
Hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya ardhi mjini Arusha hasa katika eneo la Loliondo karibu na mbuga ya kitaifa ya wanyama ya Serengeti imekodishwa kwa kampuni ya uwindaji ya Emirati iitwayo Ortello
Tangu mwaka 1992, kampuni hiyo imekuwa ikiwapeleka kwa ndege watalii matajiri zaidi kuwinda simba na wanyama wengine hali iliyowaghadhabisha wenyeji wa eneo hilo ambao ni wamaasai ambao wamezuiwa kuwalisha mifugo wao katika maeneo ya kuwinda.
Sasa serikali ya Tanzania inataka kutoa ardhi zaidi kwa wawindaji hao kwa lengo la kujenga barabara ya umbali wa kilomita 1,500 ambako wanyamapori watakuwa wakipita kwa manufaa ya kampuni hiyo ya uwandaji.
Mpango huo utawaathiri takriban watu 30,000 watakaoachwa bila makao na pia kuwaathiri maelfu ya wengine, ambao huwalisha mifugo wao katika maeneo hayo wakati wa msimu wa kiangazi.
Wamaasai wameghadhabishwa mno na hata kufanya maandamano, wakisema kuwa maisha yao yataathirika pakubwa.
Zaidi ya asilimia ya 90 ya wakaazi wa Loliondo ni wa Maasai ambao hutegemea kuwalisha mifugo wao nyasi kutoka eneo ambalo serikali inanuia kuwakodishia waarabu.
"bila Ardhi hatuwezi kuishi,'' anasema mama Naishirita Tenemeri, mwenye watoto watatu.
Bi Tenemeri anafuga Ng'ombe na Mbuzi eneo la Loliondo, ili kuwanunulia chakula na kuwalipia karo ya shule wanawe.
Wengine walitembea kwa siku nyingi kuonyesha ghadhabu yao kwa kujiondoa katika chama tawala cha CCM kama wanachama.
"ikiwa sina ardhi, sina mahala pa kujifungulia watoto wangu,'' alisema Bi Morkelekei Gume,akitupa kadi yake ya uwanachama wa CCM chini .
"mwanangu yuko katika shule ya upili, kwa sababu ya nyasi zinazotoka hapa.''
''Ikiwa wanataka ardhi yangu wanaweza kuniua.''
Mwanamke mmasaai anashikia bango linalosema
"tutapigania ardhi yetu hadi mwisho wake.'' Wanawake hapa ndio wamekuwa
wakisikika zaidi katika maandamano yao.
Wanawake wamekuwa wakisikika zaidi, wameathirika zaidi kutokana na hatua ya serikali kuwafukuza, wakiachwa bila kazi kuwalea watoto wao kwa hali ngumu wakati wanaume wakienda katika sehemu za miji ambako wanapata kazi kama walinzi.
Pia wameongoza maandamano tangu viongozi wao wa kisiasa waliopinga mpango wa ujenzi wa barabara waliokuwa wamesema wataondoka katika chama tawala kukosa kutimiza ahadi zao.
Eneo la Loliondo lina wanyama wengi wa porini na hivyo kuvutia watalii ingawa sio wengi. Linapakana na mbuga ya wanyama ya Maasai Mara iliyoko Kenya pamoja na hifadhi ya wanyama ya Ngorongoro.
Waziri wa utalii Khamis Kagasheki anatetea hatua ya serikali kutaka kuwaondoa wamasaai katika eneo hilo akisema kuwa mradi huo utasaidia katika kuendeleza uhifadhi kwani Maasai wametumia ardhi hiyo vibaya.
Ni nadra kwa wamaasai kuwinda wanyama na hutumia ardhi kuzuia baadhi ya wanyama kujifungulia huko kwani ni tisho kwa mifugo wao.
Mashirika 13 ya kijamii kutoka kote nchini Tanzania, yamesema kuwa wamaasai, wana vibali vichache sana vya kumiliki ardhi, na kuwa serikali inawapotosha watu
Viongozi wa jamii hiyo wanapanga kwenda mahakamani kuishtaki serikali, lakini wanahofia kuwa huenda swala hilo likakosa kutatuliwa haraka kwani kuna kesi moja iliyowasilishwa mwaka 2009 na haijapata ufumbuzi hadi wa leo.
Wa Maasai watetea ardhi yao Tanzania
Kwa karne nyingi, (Savanna) katika eneo la Arusha lilikuwa makao kwa watu wa jamii ya wamaasai lakini siku hizi mtu sasa anaweza kudhania yuko Dubai moja ya nchi za milki za kiarabu.
Hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya ardhi mjini Arusha hasa katika eneo la Loliondo karibu na mbuga ya kitaifa ya wanyama ya Serengeti imekodishwa kwa kampuni ya uwindaji ya Emirati iitwayo Ortello
Tangu mwaka 1992, kampuni hiyo imekuwa ikiwapeleka kwa ndege watalii matajiri zaidi kuwinda simba na wanyama wengine hali iliyowaghadhabisha wenyeji wa eneo hilo ambao ni wamaasai ambao wamezuiwa kuwalisha mifugo wao katika maeneo ya kuwinda.
Sasa serikali ya Tanzania inataka kutoa ardhi zaidi kwa wawindaji hao kwa lengo la kujenga barabara ya umbali wa kilomita 1,500 ambako wanyamapori watakuwa wakipita kwa manufaa ya kampuni hiyo ya uwandaji.
Mpango huo utawaathiri takriban watu 30,000 watakaoachwa bila makao na pia kuwaathiri maelfu ya wengine, ambao huwalisha mifugo wao katika maeneo hayo wakati wa msimu wa kiangazi.
Zaidi ya asilimia ya 90 ya wakaazi wa Loliondo ni wa Maasai ambao hutegemea kuwalisha mifugo wao nyasi kutoka eneo ambalo serikali inanuia kuwakodishia waarabu.
"bila Ardhi hatuwezi kuishi,'' anasema mama Naishirita Tenemeri, mwenye watoto watatu.
Bi Tenemeri anafuga Ng'ombe na Mbuzi eneo la Loliondo, ili kuwanunulia chakula na kuwalipia karo ya shule wanawe.
Wa Maasai wana historia ya kupoteza ardhi yao nchini Tanzania tangu wazungu walipowahamisha kutoka mbuga ya Serengeti mwaka 1959.
Mapema mwezi huu, Bi Tenemeri, akiwa amejifunga shuka yake nyekundu, alijiunga na watu 1,000 wengi wao wakiwa wanawake chini ya miti ya mivule, katika kijiji cha Olorien kupinga mipango ya serikali kuuza ardhi yao.Wengine walitembea kwa siku nyingi kuonyesha ghadhabu yao kwa kujiondoa katika chama tawala cha CCM kama wanachama.
"ikiwa sina ardhi, sina mahala pa kujifungulia watoto wangu,'' alisema Bi Morkelekei Gume,akitupa kadi yake ya uwanachama wa CCM chini .
"mwanangu yuko katika shule ya upili, kwa sababu ya nyasi zinazotoka hapa.''
''Ikiwa wanataka ardhi yangu wanaweza kuniua.''
Wanawake wamekuwa wakisikika zaidi, wameathirika zaidi kutokana na hatua ya serikali kuwafukuza, wakiachwa bila kazi kuwalea watoto wao kwa hali ngumu wakati wanaume wakienda katika sehemu za miji ambako wanapata kazi kama walinzi.
Pia wameongoza maandamano tangu viongozi wao wa kisiasa waliopinga mpango wa ujenzi wa barabara waliokuwa wamesema wataondoka katika chama tawala kukosa kutimiza ahadi zao.
Eneo la Loliondo lina wanyama wengi wa porini na hivyo kuvutia watalii ingawa sio wengi. Linapakana na mbuga ya wanyama ya Maasai Mara iliyoko Kenya pamoja na hifadhi ya wanyama ya Ngorongoro.
Waziri wa utalii Khamis Kagasheki anatetea hatua ya serikali kutaka kuwaondoa wamasaai katika eneo hilo akisema kuwa mradi huo utasaidia katika kuendeleza uhifadhi kwani Maasai wametumia ardhi hiyo vibaya.
Lakini wasomi wanasema kuwa jamii ya wamaasai kawaida hawaathiri wanyamapori.
"nina swali moja kubwa kwa wanaosema kuwa wamaasai ni tisho kubwa kwa wanyamapori kuliko kampuni hiyo ya kiarabu ya OBC," alisema Benjamin Gardner wa chuo kikuu cha Washington na ambaye amesomea maswala ya ardhi miongoni mwa wamaasai kwa miongo miwili.Mashirika 13 ya kijamii kutoka kote nchini Tanzania, yamesema kuwa wamaasai, wana vibali vichache sana vya kumiliki ardhi, na kuwa serikali inawapotosha watu
Viongozi wa jamii hiyo wanapanga kwenda mahakamani kuishtaki serikali, lakini wanahofia kuwa huenda swala hilo likakosa kutatuliwa haraka kwani kuna kesi moja iliyowasilishwa mwaka 2009 na haijapata ufumbuzi hadi wa leo.
No comments:
Post a Comment