BAADA ya maneno kibao katika uhusiano wao, hatimaye wasanii wa filamu
na muziki Bongo, Hamis Ramadhan Baba ‘H. Baba‘ na Flora Mvungi,
wametiza ahadi yao ya kufunga ndoa ya nguvu.
Wawili hao walifungishwa ndoa na Shehe Maulid katika Msikiti wa Kibo,
uliopo Ubungo, Dar, Jumamosi iliyopita na baada ya ndoa kufungwa
sherehe ilifanyika nyumbani kwa akina Flora maeneo ya Kibo.
“Tumefurahi
sana na tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumetimiza ndoto yetu kwani maneno
yamesemwa mengi sana juu ya uhusiano wetu lakini Mungu ameendelea
kutuweka pamoja mpaka tumefunga ndoa,” alisema Flora.