SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG
Wednesday, 15 May 2013
SIMBA VS YANGA JUMAMOSI: HIVI NDIO VIINGILIO NA MWAMUZI ATAKAYEAMUA MCHEZO HUO
Kiingilio
cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na
Yanga itakayochezwa Jumamosi (Mei 18 mwaka huu) kitakuwa sh. 5,000.
Kiingilio hicho kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.
Kwa
upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi
ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B
itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja
itapatikana kwa sh. 30,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni.
Mwamuzi
wa mechi hiyo atakuwa Martin Saanya kutoka Morogoro ambapo atasaidiwa
na Samuel Mpenzu wa Arusha, na Jesse Erasmo kutoka Morogoro. Mwamuzi wa
akiba ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam.
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Leslie Liunda.
Subscribe to:
Posts (Atom)