kaa tayari kwa blog yangu mpya ya fashion JACK255.BLOGSPOT.COM....

SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG

Wednesday, 23 April 2014

Shabiki wa Liverpool aliyefuga nywele miaka 11 akiapa kutokata mpaka Liverpool awe bingwa EPL

uka1_9644Shabiki wa mmoja wa klabu ya Liverpool huko nchini Kosovo ameweka kiapo kilichodumu kwa miaka 11 juu ya klabu ya Liverpool.
Shabiki huyo aliyefahamika kwa jina la Ukë Krasniqi aliweka kiapo cha kutokukata nywele zake miaka 11 –  kuanzia mwaka 2003 mpaka leo hii, akiapa kwamba hatozikata nywele hizo mpaka pale Liverpool itakapotwaa ubingwa wa Uingereza maarufu kama Barclays Premier League.
Hivi sasa story hiyo ya raia huyo wa Kosovo imetengeneza headlines na gazeti la Kosovo Republika.mk, limemfanyia mahojiano Ukë Krasniqi na haya ndio aliyosema:
“Tangu mwaka 2003 nilianza kufuga nywele zangu…Mpaka sasa Liverpool imeshinda kila kombe lakini sio Premier League. Sasa tumekaribia kushinda ubingwa huo. 
Hata kama tutangazwa mabingwa mapema, nitaendelea kufuga nywele zangu mpaka May 11. Nataka kushangilia na nywele zangu  wakati Steve Gerrard atakapobeba kombe kwa mara ya kwanza, kisha baada ya hapo nitakata.”

Hiki ndio kiasi cha fedha alicholipwa David Moyes baada ya kutimuliwa

article-2609490-1D411CD200000578-628_634x505Siku moja baada ya kutimuliwa kutoka kwenye kibarua cha kuifundisha klabu ya Manchester United imefahamika kwamba kocha David Moyes atalipwa fidia kutokana na klabu hiyo kuvunja mkataba wa miaka sita walioingia mwaka jana mwezi wa tano.
David Moyes atalipwa fidia ya £5million baada ya kufukuzwa kazi na Manchester United – ikiwa ni kipengele cha makubaliano ya mkataba wake na klabu hiyo.
Katika mkataba wa Moyes na United kulikuwa na kipengele kinachoeleza ikiwa Manchester United ingefeli kufuzu kucheza Champions League msimu huu basi ikatokea United wakaamua kusitisha mkataba wake basi fidia isingezidi mshahara wake wa miezi 12 ambao ni £5million.

AJALI MBAYA ILIYOTOKEA IRINGA


Taxi ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa katika eneo la tukio, huku askari polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu katika eneo la tukio

Daladala aina ya Coster yenye namba za usajiri T.960 AQY inayofanya safari zake za Kibwabwa mjini Iringa mara baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu Tipa, lenye namba SM 3363 katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha Bibi.