SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG
Monday, 27 May 2013
FEZA KESSY NA NANDO WAIWAKILISHA TANZANIA NDANI YA BBA 2013
Big Brother Africa 2013 "The Chase" imeanza kwa kasi usiku wa jana (26 may) na msanii Feza Kessy na Nando ndio wanaoiwakilisha Tanzania. kwa mujibhu wa story yake mwenyewe Nando ni mtanzania anaeishi marekani lakini ilimbidi aombe hela kwa marafiki zake kwa ajili ya kupata ticket ya kuja Tanzania kufanya usahili wa BBA, amesema kama angekosa nafasi ya kuiwakilisha Tanzania asinge juta maana pia alikua hajamuona bibi yake kwa miaka mingi, kwahiyo angekuwa kaitumia nafasi hiyo kuja kumuona bibi yake.
TAIFA STARS NDANI YA SUTI MPYA ZILIZOANDALIWA KWA AJILI YAO NA MBUNIFU SHERIA NGOWI
Wachezaji wa Taifa Stars na benchi la ufundi katika picha ya pamoja wakionesha suti zao. |
Wachezaji wa Taifa Stars, benchi la ufundi na maofisa wakuu wa TBL katika picha ya pamoja wakati wa kuonesha suti mpya |
Wachezaji wakifurahia huku wakishangiliwa baada ya kuonesha suti zao mpya. |
John Bocco na Erasto Nyoni |
Wageni waalikwa wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya Kilimanjaro Premium Lager kukabidhi suti mpya kwa Taifa Stars. |
TAIFA STARS WAONDOKA KWENDA KUIWEKEA KAMBI MOROCCO ADDIS ABABA
Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kuondoka leo (Mei 26
mwaka huu) usiku kwenda Addis Ababa, Ethiopia ambapo itaweka kambi na
kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya kwenda Morocco.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka saa 5 usiku kwa
ndege ya EgyptAir ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 chini ya nahodha wake
kipa Juma Kaseja.
Timu
hiyo ikiwa Ethiopia, Juni 2 mwaka huu itacheza mechi ya kirafiki dhidi
ya Sudan ambapo siku inayofuata itaondoka kwenda Marrakech, Morocco kwa
kupitia Cairo, Misri. Mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya
wenyeji Morocco itachezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.
Mbali
ya nahodha Kaseja, wachezaji wengine wanaoondoka katika kikosi hicho
ambacho kina wiki sasa tangu kingie kambini jijini Dar es Salaam ni
Mwadini Ally na Ally Mustafa ambao wote ni makipa.
Wengine
ni Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Aggrey Morris, Haroub Nadir, Mwinyi
Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum
Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya,
Athuman Idd na Haruni Chanongo.
Wachezaji
Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu ambao wako na timu yao ya TP Mazembe
ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo watajiunga moja kwa moja na Stars
jijini Marrakech, Juni 4 mwaka huu wakitokea Maputo, Msumbiji mara baada
ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Liga Muculumana ya huko.
Katika
msafara huo wa Ethiopia benchi la ufundi la Stars linaundwa na Kim
Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi),Juma Pondamali
(Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja wa timu), Dk. Mwanandi
Mwankemwa (Daktari), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred
Chimela (Mtunza vifaa).
DJ NOBLE:NEW BONGO HOT MIXING 2013
UNAWEZA KUMCHEKI THROUGH:
Phone no:0717791274
Bbm pin:21A8EA87
Email:Yusuphjuma54@yahoo.com
Facebook:Dj noble
BREAKING NEWS: NEYMAR ATHIBITISHA ANAJIUNGA NA BARCELONA
BARCELONA wamefanikiwa kushinda mbio za kumsaini nyota wa Brazil Neymar kwa ada ya uhamisho ya £20million kwa mkataba wa miaka mitano.
Mshambuliaji huyo sasa anaelekea barani ulaya baada ya Santos kukubali kumuuza nyota wao waliomng'ang'ania kwa miaka mingi.Akiandika kwenyepage yake ya Instagram, Neymar alisema: "Nimeongea na marafiki na familia. Jumatatu nitajiunga na Barcelona."
Mabosi wa Barca walienda Sao Paolo kwa mazungumzo mazito kuhusu usajili wa mbrazili huyo, na wakafanikiwa kuwashawishi Santos kumuuza Neymar ambaye angeweza kuondoka bure mwezi Julai.
Neymar alitaka muda kufikiria ofa nyingine kutoka kwa wapinzani wa Barca Real Madrid lakini mwishoni akaamua kwenda Nou Camp.
Kwa usajili huu sasa Neymar atacheza atajiunga na star wa Argentina Lionel Messi na kuunda safu ya ushambuliaji inayotisha barani ulaya.
Neymar ameifungia Santos mabao 138 kwenye mechi 229 tangu mwaka 2009.
Subscribe to:
Posts (Atom)