Mtangazaji Sakina wa Clouds TV
ameongea na millardayo.com akiwa Zanzibar sasa hivi Msibani kwa Msanii
wa siku nyingi Bibi Kidude na hapa namkariri akisema “Anatarajiwa
kuzikwa kesho April 18 2013 Zanzibar saa saba mchana pembeni ya kaburi
la Baba yake , japo kuna habari za chini ambazo bado hazijathibitishwa
kwamba kuna uwezekano akaagwa kwanza kwenye Uwanja wa Karume alafu
azikwe saa kumi jioni”
“Bibi Kidude hakuwahi kupata
mtoto lakini nimekutana na kijana mmoja aitwae Baraka ambae kwa sasa
umri umekwenda kidogo, anatambulika kama ndio mwanae Bi Kidude kwa
sababu alimlea toka akiwa na miezi mitatu, japo maziwa yalikua hayatoki,
imefahamika aliwahi kumnyonyesha ziwa lake” – Sakina
Kwa kumalizia, Sakina anasema
“Baraka akiwa na umri wa miaka 13 ndio aligundua kwamba Bibi Kidude ni
shangazi yake, baba Baraka alimpa Bi Kidude Baraka baada ya kuona hakuwa
amepata mtoto, hapa kwenye msiba watu ni wengi sana na inakua ngumu kwa
mgeni kujua ni nyumba ipi yenye msiba”
No comments:
Post a Comment