Mbunge mchungaji Peter Msigwa |
Polisi waliotoka kumkamata mbunge Msigwa leo |
Gari ya mbunge Msigwa kabla ya kukamatwa leo kwa kuhusishwa na vurugu
MASAA zaidi ya 6 ya mapambano
kupiga mabomu ya machozi na kurushiana mawe kati ya
wafanyabiashara ndogo ndogo (machinga ) na askari
wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Iringa
yaishia pabaya kwa jeshi la polisi kumkamata
mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa
(chadema) na watu wengine zaidi ya 60
Polisi watumia mabom ya
machozi kutawanya machinga wapiga mabomu hadi stendi kuu ya
mabasi abiria walazimika kutimua mbinu na kuacha
mizigo yao katika magari huku machinga hao wakitumia
mawe na kuchoma mataili moto barabarani kuvunja vioo vya
gari la Zimamoto na kuharibu mali mbali mbali kama njia ya
kupambana na polisi
Tukio hilo la Mapambano kati
ya machinga na polisi lilitokea leo kuanzia muda wa saa 3
asubuhi na kuendelea hadi saa 8 mchana katika eneo la
Mashine tatu mjini Iringa na maeneo mbali mbali ya mji
wa Iringa .
Mtandao huu wa na simonbango.blogspot.com
ambao ulituma wawakilishi zake eneo la tukio toka saa
12 za asubuhi ya jana alishuhudia kundi kubwa la askari
wa FFU wakiwa na gari la maji ya kuwasha ambao wakesha
wakilinda eneo hilo .
Askari huo
walilazimika kukesha wakilinda eneo hilo kufuatia kauli
ya mbunge Msigwa aliyoendelea kuitoa katika mikutano
yake ya hadhara mjini hapa kuwhamasisha machinga hao
ambao Halmashauri ya Manispa ya Iringa iliwahamisha
eneo hilo la mashine tatu na kuwapeleka eneo la Mlandege kabla
ya mbunge Msigwa kuwahamasisha kurejea tena eneo hilo.
Kabla ya mbunge Msigwa
kufika eneo hilo majira ya saa 3 asubuhi machinga hao
ambao walikuwa wamejikusanya makundi madogo madogo
bila kupanga biadhaa zao walisikika wakidai
kumsubiri mbunge Msigwa kama alivyopata kuwaahidi kuwa
atafika eneo hilo kuungana nao kwa kuwa machinga mpya .
Hata hivyo baada ya
mbunge huyo kufika akiwa na gari lake la kibunge ambalo
lilikuwa lilikokota tela la kuhifadhia mizigo alisimama
eneo hilo na kuendeleza msimamo wake wa kuwataka machinga
kupambana na baada ya muda alitoweka eneo hilo kabla ya
polisi kuanza kuwatawanya machinga hao kwa mabomu ya machozi
.
Wakizungumzia hali hiyo
ambayo ni ya kwanza kutokea katika mji wa Iringa wakazi
wa mji wa Iringa walisema kuwa mbunge na
viongozi wengine wa serikali wanapaswa kulaumiwa
kwa kushindwa kutumia njia nzuri ya kukutana kwa ajili
ya kumaliza mvutano huo ambao unaendeshwa kisiasa
zaidi.
Festo Sanga alisema
kuwa hali ilipofikia ni mbaya zaidi na hivyo
busara zinahitajika kwa ajili ya kutatua tatizo
hilo ikiwa ni pamoja na kutazama eneo zuri kwa ajili ya
machinga bila kuendelea kuonyeshana ubabe .
Sanga alisema kuwa
machafuko yaliyojitokeza leo ni machafuko ambayo wakazi
wa mji wa Iringa walikuwa wakishuhudia katika
vyombo vya habari katika mikoa mingine
ukiacha lile la Septemba 2 mwaka jana lililotokea
kijiji cha Nyololo kati ya wafuasi wa Chadema na polisi na
kupelekea kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya
waandishi wa habari mkoa wa Iringa marehemu Daud Mwangosi.
“Kweli katika hili mbunge wetu
hapaswi kuendelea kulazimisha machinga kuvunja sheria
ila anayo nafasi ya kukutana na viongozi wenzake ili
kutafuta suluhu ya jambo hilo vinginevyo wanaoteseka na
machinga na wale waliokamatwa kwa vurugu hizo
ujue wengi waliopigwa mabomu ya machozi si machinga
wengine walikuwa wasafiri na badhi yao walikuwa
wakielekea makanisani ”
KUhusu kukamatwa kwa
mbunge huyo na kuhojiwa na polisi juu ya vurugu hizo
Sanga alisema kwa upande wake analipongeza jeshi la
polisi kwa kutumia busara zaidi ya kumkamata
mbunge kama mhusika mkuu na kuliomba jeshi
la polisi kuwaachia wananchi waliokamatwa kwa
vurugu hizo.
Huku Sarah Kalinga
alidai kuwa chanazo cha machafuko hayo ni mvutano kati ya CCM
na Chadema na kuwa ilipaswa vyama vyote viwili
kukutana na kuwasaidia machinga badala ya
kuwanyanyasa kwa kutumia nguvu kuwabana .
Hata hivyo alisema
wao kama walalahoi wanampongeza mbunge wao kwa kuonyesha kuwapigania japo
haungi mkono njia inayotumiwa na mbunge ya
kuwahamasisha kuvunja sheria na kuwa matatizo na
majeraha wanapata wao wananchi na sio mbunge.
Awali mbunge mchungaji
Msigwa kabla ya kukamatawa na jeshi la polisi alitoweka
katika mazingira tata katika eneo hilo la mashine tatu
na kuibukia eneo la chuo kikuu cha Tumaini Iringa ambako kulikuwa
na harambee ya kuchangia Kanisa na mgeni rasmi akiwa
waziri mkuu mstafu Frederick Sumaye na mara baada ya shughuli
hiyo kumalizika ndipo alipokamatwa na polisi na kufikishwa kituo
cha polisi.
Kabla ya kukamatwa kwake
mbunge Msigwa alizungumza na mwandishi wa habari hizi na kuwa yupo
tayari kukamatwa wakati wowote na kuwa kamwe
ataendelea na msimamo wake wa kuwataka Machinga
kufanya biashara eneo hilo.
Mbali ya kukamatwa
kwa mbunge Msigwa kwa kuhusishwa na vurugu hizo
pia jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia
watu wengine zaidi ya 60 akiwemo aliyekuwa kampeni
meneja wa Chadema jimbo la Iringa mjini na mgombea
udiwani kata ya kwa Kilosa Abuu Changawa Majeck.
Huku idadi ya majeruhi
waliojeruhiwa kwa kupigwa mawe na machinga na badhi ya
machinga waliokamatwa kwa vurugu hizo pia wakijeruhiwa
vibaya wakati wakipambana na polisi hao.
Taarifa kutoka
jeshi la polisi zilizothibitishwa na kamanda wa polisi mkoa
wa Iringa Michael Kamuhanda zinadai kuwa watu zaidi ya
60 ndio wamekamatwa hadi sasa na jitihada za
kuwasaka wengine waliohusika katika vurugu hizo ambazo
zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali za wananchi unaendelea.
Huku akidai mali mbali
mbali zimeharibiwa likiwemo gari hilo la zimamoto mjini Iringa
pamoja na uharibifu mwingine mdogo mdogo wa mali
za wananchi .
Jeshi hilo la polisi
limesema kamwe halipo tayari kumwachia mbunge Msigwa kwa leo hadi hapo
atakapofikishwa mahakamani Kesho
| |||