SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG
MTANZANIA FEZA AZIDI KUNGA'ARA BIG BROTHER AFRICA....AUKWAA UKUU WA KAYA
Tunaenda vizuri, bahati inaonekana kutuangukia watanzania kwani
mshiriki Feza jana ameukwaa ukuu wa kaya ama kwa lugha ya ki-big brother
‘Head of House’.
Ilikuwaje?
Baba mwenye nyumba, biggie, alitoa task ambayo washiriki walitakiwa
kuelekea bustanini na kuchagua box, ambaye angechukua box la ushindi ndo
huyo angekuwa mkuu wa kaya. Kama zali, bahati hiyo ilimuangika mrembo
Feza. Washiriki wenzie akiwemo mtanzania Nando, walimkumbatia kwa furaha
kama ishara ya kumpongeza.
Iko hivi, ukichaguliwa kuwa mkuu
wa kaya, unauwezo wa kumuokoa mtu ambaye anakuwa amependekezwa atoke
katika wiki hiyo. Usipofanya hivyo basi wewe mwenyewe unawekwa
kikaangoni.
Feza alitumia nafasi hiyo kumuokoa Elikem ambaye
ni mshiriki kutoka Ghana na kumuweka kikaangoni Betty kutoka Ethiopia.
Hiyo ni siri ambayo Feza inabidi aitunze hadi siku ya Jumapili wakati wa
Eviction.
Hii issue ya kumuokoa Elikem wa Ghana, je ni dalili ya shemeji shemeji mbona wazima taa? Endelea kufuatilia..