Jemma Benjamini |
Kwa mujibu wa mtandao wa telegraph wa Uingereza,
Msichana Jemma Benjamini raia wa uingereza ambae alikuwa
mwanafunzi
wa chuo kikuu, alipoteza maisha baada ya kupigwa busu na mwanafunzi
mwenzake aliyefahamika kwa jina la Daniel Ross (21) nyumbani kwao na
kijana huyo baada ya kutoka kwenye mtoko wa usiku kama marafiki.hiyo
ilikuwa ni April 2009
Lakini katika mishemishe za kukaa pamoja
kwa dakika kadhaa kwenye sofa
wakibadilishana maelezo kadhaa walijikuta wakikiss taratibu,
muda mfupi baada ya kiss hiyo Daniel alimuona
mwenzake analegea taratibu huku macho yake yakiishiwa nguvu na kisha kutulia kabisa.
Hali hiyo ilianza kumtisha kijana huyo ambae anasema
hawakuwahi kuwa na mahusiano ya mapenzi kabla, na hiyo ilitokea tu wakajikuta wanakiss.
Baada ya hapo alimpigia simu mama yake
kisha akapiga simu kuomba msaada zaidi wa matibabu
na ambulance ilifika na kumkimbiza
hospital ambapo aligundulika kuwa tayari alikuwa ameshafariki.
Ripoti ya uchunguzi ya daktari ilionesha kuwa
hakukua na sababu zozote za kimatibabu zilizopelekea kifo chake. Na kwamba kifo cha msichana huyo kimetokana na matatizo
yanayojulikana
kama Sudden Adult Syndrome (SADS), tatizo dogo la moyo linaloaminika
kuwauwa watu takribani 500 kila mwaka nchini uingereza.