Wengi tulidhani hili swala limeisha hasa baada ya wahusika
wote kuzungumza akiwemo mlalamikaji Dayna Nyange,
producer Sheddy Clever wa Burn Records aliyeitengeneza
beat hiyo iliyoleta mzozo, na Diamond Platnumz
aliyeitumia beat hiyo katika single yake mpya ambayo ni
talk of the town ‘My Number One’.
Sheddy Clever ameongea exclusive na Bongo5 na kusema
kuwa pamoja na kuwa yeye ndiye producer na mmiliki wa
beat hiyo iliyozua utata lakini Dayna amemshitaki COSOTA
kwa kumuibia beat aliyotumia Diamond katika ‘My Number
One’.
Sheddy amesema alipokea simu kutoka COSOTA na kupewa
taarifa kuwa anahitajika kufika katika ofisi zao
Jumatano hii (September 25) kwaajili ya kesi hiyo.
Haya ndio maelezo ya Sheddy Clever:
“Juzi ilikuwa tarehe 14 nimepigiwa simu na namba ngeni
ambayo siijui wakajitambulisha wao ni COSOTA,
nikaambiwa nabarua yangu pale njiifuate inipe muongozo
kwamba nahitajika pale. Basi sikuwa nashaka wala na
hofu yoyote kwasababu mi ni mtu ambaye nafanya kazi na
COSOTA ni watu ambao wapo kwaajili ya kazi yangu ya
muziki.
Kwahiyo nikaenda nimefata hiyo barua kuja kufungua ile
barua ni kuhusu mambo ya Dayna. Dayna ameenda
ameshtaki amesema kwamba ile beat ameibiwa kwahiyo
mpaka dakika hii mi sielewi kwamba ana matatizo gani
huyo dada anasema kwamba ile beat kaibiwa na je, unajua
kwamba ni makosa kumuita mtu mwizi kwahiyo anaweza
kufunguliwa mashtaka kwanini amuite mtu mwizi, je
anauhakika gani au ushahidi gani ile beat kaibiwa.
Kwahiyo nimeambiwa niende tarehe 25 ili niende
nikaskilize inakuwaje, kwahiyo mi ntaenda kuskiliza
tarehe 25 tujue inakuwaje ili tuweze kupata muafaka wa
hili swala sababu mi sipendi haya matatizo….kwasababu
naona yeye anataka liwe tatizo kwasababu mi naona
limeisha…mi nahisi linaendelea kuwa kubwa zaidi, kwahiyo
kama yeye anahitaji liwe kubwa basi litakuwa kubwa zaidi
kama anahitaji yaishe basi yaishe”.
Sheddy aliongeza kuwa toka Dayna aanze kulalamika
kupitia mitandao hajawai kumtafuta hata mara moja ili
angalau amuulize chochote, zaidi ya kusoma habari zote
katika vyombo vya habari na mpaka alipokuja kupokea
barua ya kuitwa COSOTA.
Sheddy amesema katika barua hiyo wameitwa yeye,
Diamond Platnumz pamoja na meneja wa studio ya Burn
Records aitwaye D.Manyuti. Hata hivyo Sheddy aliongeza
kuwa Diamond amesema hatahudhuria.
Mpaka habari hii inaenda hewani nimejaribu kumtafuta
Dayna Nyange ili kuthibitisha kama ni kweli alifikisha
malalamiko yake COSOTA kuhusu swala hilo lakini simu
yake haikupokelewa
No comments:
Post a Comment