kaa tayari kwa blog yangu mpya ya fashion JACK255.BLOGSPOT.COM....

SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG

Monday, 7 October 2013

MAMA WEMA AMWANGUSHIA PATI ZAMARADI SIKU YA BIRTHDAY YAKE

Mama wa Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu, amemfanyia kufuru mtangazaji wa Kipindi cha Take-One, kinachorushwa kupitia Clouds TV, Zamaradi Mketema kwa kumwangushia bonge la pati ya siku yake ya kuzaliwa.
Mariam Sepetu akiwa na Zamaradi Mketema wakati wa pati ya siku yake ya kuzaliwa.
Mpango mzima ulijiri mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa mama huyo Sinza-Mori jijini Dar.
Mama Wema alimfanyia mtangazaji huyo sherehe hiyo kama ‘sapraizi’ ambapo alimuomba afike nyumbani  kwake majira ya saa 1:00 usiku akimwambia kuna kitu alitaka kuzungumza naye.
Zamaradi ambaye hivi karibuni aliibuka kidedea na kuwa mtangazaji mwenye mvuto runingani kupitia gazeti tumbo moja na hili, Amani, hakusita na kuamua kumuibukia bi‘mkubwa huyo.
Alipofika nyumbani hapo akiambatana na mwanahabari wetu, alikutana na meza iliyosheheni misosi na vinywaji mbalimbali kisha mama huyo akamkaribisha huku akimwambia ilikuwa spesho kwa ajili ya siku yake ya kuzaliwa.
Kitendo hicho kilimfanya Zamaradi kuangua kilio hasa wakati wa kukata keki kwani hakuamini alichokutana nacho.
“Ni jambo kubwa sana kwangu maana hii ndiyo ‘bethidei’ ya kwanza kuifanya bila mama yangu mzazi lakini leo najisikia sijapungukiwa kwa sababu nina mama mwingine anayenithamini,” alisema Zamaradi.
Kwa upande wa mama Wema, alisema kuwa anamuona Zamaradi kama mtoto wake hivyo aliamua ‘kumsapraizi’ ili ajisikie vizuri kwa vile anafahamu kabisa kuwa mama yake alitangulia mbele ya haki na yeye ni kama mama kwa mtangazaji huyo.
Baada ya kumaliza sherehe hiyo iliyokuwa fupi, Zamaradi ambaye ni rafiki mkubwa wa Wema, alielekea kwenye Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo Posta, Dar ambapo alikwenda kugonga mnuso na kukata keki nyingine pamoja na marafiki zake.

No comments: