FC Bayern wanakutana na mtihani
mgumu usiku wa leo watakapocheza dhidi ya Borussia Dortmund kwenye dimba
la Wembley jijini London. Leo ni siku ya kuondokana na mkosi mkubwa
unaowatawala mabavarians ambao ndio timu inayoongoza kwa kufungwa kwenye
UEFA Champiosn League - leo ni siku ya kufuta machungu kwa kupoteza
mechi ya fainali ya mwaka jana ambayo walistahili kushinda ingawa bahati
haikuwa upande wao.
Hii ni fainali ya kwanza ya wajerumani ambao wanastahili kuwemo kwenye fainali hiyo. Utakuwa mchezo mzuri wa kukumbukwa.
Dortmund, klabu inayoibuka kuwa na nguvu barani ulaya
Majeruhi: Mario Götze
Baada ya kusemwa kuwa kutolewa kawenye
hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wa ulaya msimu wa 2011-12, Dortmund
hatimaye wameyachukulia uamakini mashindano haya kwa gaharama ya
kupoteza ubingwa wa nyumbani.
Ingawa, mchezo wao kwenye Champions
League umekuwa wa aina yake. Nguvu, ushirikiano, mbinu za mchezo wao
zimekuwa nzuri kiasi cha kuvishinda vilabu kama Real Madrid.
Mario Götze, kiungo mchezashaji wao,
ataukosa mchezo huo kutokana na majeruhi ya misuli. Alijaribu kurudisha
fitness yake kupitia mazoezi, lakini bahati haikuwa yake na akaawambia
mchezo wake wa mwisho wa msimu huu ulikuwa pale Santiago Bernabeu. Ujuzi
ambao BVB wataukosa ni pasi muhimu, kukimbiza mpira na mashuti yenye
madhara
Wachezaji wa kuchungwa.
Kukosekana kwa Gotze kutamuacha
mchezashaji Marco Reus. Kiungo huyo mshambuliaji anaweza kufanya runs za
hatari pia kupiga mashuti na kutoa pasi za mwisho za hatari. Kazi ya
kumzuia Reus kwa hakika atapewa kiungo mkabaji wa Bayern Javi Martinez
ambaye aliweza kuwazima Iniesta na Andrea Pirlo kwenye mechi za raundi
zilizopita.
Robert Lewandowski amegeuka kuwa
mshambuliaji wa kiwango cha dunia, ameonyesha utulivu mbele ya lango la
adui ambao washambuliaji wanakosa. Ana control nzuri ya mpira, anapiga
mashuti yenye kulenga goli.
Muhimu zaidi, ni hazina ya Dortmund
kwenye kulinda lango - golikipa Roman Weidenfeller. Uwezo wake wa kudaka
uliinyima Bayern ushindi kwenye michezo kadhaa iliyopita msimu huu.
Beki wa kati Mats Hummels anaweza
akacheza mechi ya fainali pamoja na kuwa na majeruhi. Kitu cha kuvutia
kuhusu yeye ni kwamba pamoja na mlinzi kwa ujumla, lakini pia anaweza
akaigharimu timu yake kwa makosa ya kizembe.
Ilkay Gündogan ni kiungo mzuri mkabaji
ambaye anaweza kufanya dribbling vizuri kuwapita mabeki wa Bayern,
lakini sio mzuri kwa mipira ya juu ambao ndio silaha inayohitajika
kuweza kuisimamisha Bayern.
Wakati uzuri wa Dortmund inacheza vizuri
hata bila kuwa na mpira, mchezo mzuri wa kupasiana unaweza ukawadhuru
kwenye nusu yao ya uwanja. Pia wana udhaifu mkubwa kwenye mipira mirefu.
Bayern, wanapaa kwenye muda muafaka
Majeruhi: Badstuber, Kroos.
Huu ni mchezo unaomaanisha kila kitu kwa Bayern, ambayo ipo kwenye kiwango cha juu kwenye muda sahihi.
The bavarians wapo kwenye moto safari
hii kwenye ulinzi na ushambuliaji. Udhaifu wao uliowagharimu msimu
uliopita ni nguvu ya akili, udhaifu ambao umeshashughulikiwa. Sasa hivi
wana ile hali ya winning mentallity - angalia namna walivyotoka nyuma na
kuwafunga Borrusia Monchengladbach 4-3.
Franck Ribéry yupo kwenye kiwango cha
dunia akicheza winga ya kushoto, unaweza ukasema hivyo pia kwa Thomas
Muller ambaye anashughulika na majukumu ya kushambulia aliyokuwa nayo
Toni Kroos.
Bastian Schweinsteiger na kila kitu cha
kutoa kwenye mchezo huu. Ni package iliyokamilika kama mchezaji, box to
box midle, yupo kwenye kiwango cha juu sana.
Uzuri wa Bayern hivi sasa mpaka
wachezaji ambao walikuwa wavivu kama Arjen Robben wanakaba, timu yote
inakaba kwa pamoja na wanashambulia kwa pamoja.
MBINU
Mtu yoyote ambaye angeniuliza timu gani
yenye mbinu kali kati ya BVB na Real Madrid: jibu lingekuwa Dortmund.
Sio tu kwamba wanaijua vizuri Bayern Munich, bali pia ni hatari sana
kwenye mchezo wa kushambulia. Ubora wa umewaumiza wapinzaani wengi,
lakini staili yao inayofanana na Barca ndio ambayo Bayern wanaiweza
kwenye kucheza dhidi nayo.
Dortmund watahitaji kucheza mchezo wa
kupelekea mashambulizi mbele, kupitia katikati ya uwanja kwa sababu ndio
mchezo wanaouweza zaidi - wakipeleka mipira kwa Robert Lewandoski.
Kwa upande wa Bayern, mshambuliaji Mario
Mandzukic (au Mario Gomez) wataungana na mchezeshaji Thomas Müller
kuzuia mistari ya pasi kwenye kiungo kwa presha huku wakirudi nyuma
taratibu
Hii itaaminisha Dortmund itabidi watumie
zaidi winga kwenda mbele. Hivyo ikiwa BVB watapeleka mpira upande wa
kushoto Arjen Robben na Javi Martinez wata press upande huo kuzia
mashambulizi. Ikiwa watapeleka upande wa kushoto Frank Ribery na Bastian
Schweinsteiger watazuia upande huo. Hii itawasaidia Lahm na Alaba
kupambana akina Reus.
Hili linaweza kuwalazimisha BVB kutumia
mipira ya juu ambayo Bayern wanaimudu pia, hivyo kuwafanya Dortmund kuwa
na option moja tu kucheza sana mpira kwenye nusu yao ya uwanja na
kujaribu kufanya counter. Hivyo nafasi zao za kufunga zitakuwa pungufu -
au italawazimu wachezaji wa Dortmund kuwashinda wa Bayern kwenye vita
ya one-on-one au kunufaika na makosa ya wachezaji wa Bayern kama
ilivyokuwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Monchengladbach wiki
iliyopita. Lakini pia Bayrn wanaweza wakawa wamepata funzo kupitia
mchezo huo na kutoruhusu makosa yale yasijirudie dhidi ya Borrusia
Dortmund usiku wa leo pale Wembley.
Ikiwa Bayern watacheza kwenye kiwango
cha juu usiku wa leo basi itawachukua BVB kutumia vipaji binafsi zaidi
vya wachezaji kuweza kushinda.
Vita binafsi leo hii itakuwa kati ya
winga wa kushoto wa Bayern Frank Ribery vs Lukasz Piszczek. Kwa spidi
aliyonayo Mpoland huyo, na uwezo wake wa kuzuia itamchukua uwezo mwingi
sana Frank Ribery kuweza kupita.
Mara ya mwisho Bayern wameifunga
Dortmund, walimtumia zaidi Toni Kroos na uwezo wake wa kumiliki mpira -
Muller hana uwezo mkubwa wa kukaa na mpira kama ilivyo kwa Kroos hivyo
mambo yanaweza magumu kiasi.
Utabiri wangu nawapa Bayern nafasi ya
kushinda. Mafunzo waliyoyapata miaka iliyopita hasa msimu uliopita dhidi
ya Chelsea yatawapa hali ya kupigana zaidi. Hata kama wataanza
kufungwa, watashindana na kuhakikisha safari hii wanaepukana na mkosi wa
fainali ya Champions League. Dortmund wana mtindo wa kupaniki - angalia
katika mechi ya pili dhidi ya Madrid nusura waondolewe pamoja kuwa
walikuwa na hazina ya mabao 4-0.
Vikosi vinavyoweza kuanza
FC Bayern (4-2-3-1)
Neuer – Lahm, Boateng, Dante, Alaba – Martinez, Schweinsteiger – Robben, Müller, Ribéry – Mandzukic
Borussia Dortmund (4-2-3-1)
Weidenfeller – Piszczek, Subotic, Hummels, Schmelzer – Gündogan, Kehl – Blaszczykowski, Reus, Grosskreutz – Lewandowski
Location: Wembley Stadium, London
Referee: Nicola Rizzoli (Italy)
Referee: Nicola Rizzoli (Italy)