Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua mwamuzi kutoka Afrika
Kusini kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika
kati ya Tanzania (Taifa Stars) na wenyeji Morocco (Lions of the Atlas).
Mechi
hiyo ya kundi C itachezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco
kwenye Uwanja wa Grand kuanzia saa 3 kamili usiku kwa saa za Morocco.
Mwamuzi atakayechezesha mechi hiyo ni Fraser Daniel Bennett.
Bennett
atasaidiwa na Thusi Zakhele Siwela pia wa Afrika Kusini, wakati mwamuzi
msaidizi namba mbili atakuwa ni Marwa Range kutoka Kenya. Mwamuzi wa
akiba (fourth official) ni Lwandile Mfiki wa Afrika Kusini.
Kamishna
wa mechi hiyo ni Robert Mangollo-M’voulou wa Gabon wakati mtathimini wa
waamuzi (referee assessor) ni Charles Masembe kutoka Uganda.
Taifa
Stars ambayo iko chini ya Kocha Kim Poulsen, na ikidhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini katika hoteli ya Tansoma
ikiendelea kujinoa kwa ajili ya mechi hiyo ambapo kabla itajipima na
Sudan (Nile Crocodiles) Juni 2 mwaka huu jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Ratiba ya mazoezi kwa timu hiyo ni kama ifuatavyo;
Mei 22 Saa 10 jioni Uwanja wa Karume
Mei 23 Saa 1 asubuhi na Saa 10 jioni Uwanja wa Karume
Mei 23 Saa 10 jioni Uwanja wa Karume
Mei 25 Saa 1 asubuhi na Saa 10 jioni Uwanja wa Karume
Mei 26 Saa 3 asubuhi Uwanja wa Karume