kaa tayari kwa blog yangu mpya ya fashion JACK255.BLOGSPOT.COM....

SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG

Friday, 27 September 2013

HIYU NDO MSANII WA BONGO MOVIE ALIYEZOMEWA BAADA YA KUKATIZA MTAANI NA NGUO YA NUSU UTUPU

MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Tamrina Posh ‘Amanda’ amejikuta katika wakati mgumu wa kuzomewa kutokana na kukatiza kitaa akiwa na nguo iliyombana na kuonesha makalio yake yaliyojazia.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, tukio hilo lilichukua nafasi Ijumaa iliyopita maeneo ya Mwenge, jijini Dar ambapo msanii huyo alikuwa ameenda kwa ajili ya kununua mahitaji mbalimbali ndipo kundi la wanaume wakware lilipoanza kumzomea.

Tukio hilo lilimfanya Amanda apoteze amani ghafla na kuamua kutimka zake eneo hilo huku akiwashangaa. Paparazi wetu hakuwa nyuma, alimpigia simu na kumuuliza kulikoni?

“Daah! Ilikuwa kero kweli, wanaume wazima wanaacha kazi zao na kuanza kunizomea huku wakiniambia kuwa ni dawa za Kichina. Lakini ukweli ni kuwa hii ni asili yangu na si Mchina,” alisema Amanda.

No comments: