*Sasa ni kipofu, adai serikali imemtelekeza Na Richard Konga, Arusha TINDIKALI inaweza kuwa silaha hatari sana na haifai hata kidogo katika jamii, wanaokutwa nayo ingefaa wafungwe kifungo cha maisha kwani wanapoitumia vibaya huleta madhara yasiyoelezeka.
Elisha Kombe kabla na baada ya kumwagiwa tindikali.
Kuthibitisha hayo tunawaletea maelezo ya Elisha Kombe aliyekuwa Afisa
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Kitengo cha Upelelezi mkoani
Mwanza, aliyemwagiwa tindikali akiwa katika majukumu ya kikazi mkoani
humo.
Miaka 15 iliyopita alikuwa mchapakazi na tena mtanashati na
nadhifu mwenye viungo kamili na alikuwa akifanya kazi yake kwa umakini
mkubwa lakini leo, anaililia serikali kwa kile alichodai kumtelekeza
baada ya kumwachisha kazi kutokana na tukio hilo lililomfanya awe
kipofu.
Kombe alikutana na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki
iliyopita jijini Arusha ambapo anaishi na kaka yake, George Kombe baada
ya kunusurika kifo kutokana na kumwagiwa tindikali wakati alipokuwa
Mwanza kwa shughuli maalumu za kikazi.
Akisimulia mkasa huo wa
kumwagiwa tindikali, Kombe alisema: “Nilipata uhamisho kutoka Makao
Makuu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania Dar es Saalam (TRA) Septemba, 1997
kwenda mkoani Mwanza kwa ajili ya kazi maalumu ya ukaguzi na kudhibiti
mianya ya ukwepaji wa mapato na magendo kwa baadhi ya wafanya biashara
wasio waaminifu.
“Nikiwa Mwanza nilishuhudia mianya hiyo ya ukwepaji
wa mapato kwa baadhi ya wafanya biashara waliokuwa wakitumia usafiri wa
majini na baadhi ya meli na boti zilikuwa zikisafirisha bidhaa kwa njia
isiyo halali sambamba na magari yaliyokuwa yakitumika nchi kavu.
“Pamoja na upinzani niliokuwa naupata vikiwemo vishawishi mbalimbali ili
niweze kupunguza kasi ya utendaji niliokuwanao lakini nilikuwa na
msimamo wa kutekeleza majukumu yangu ya kikazi kwa haki kama
nilivyoagizwa na viongozi wangu,” alisema Kombe.
Aliongeza
kuwa hali hiyo iliashiria kujengeka kwa hali ya chuki kwa baadhi ya
mitandao ya wafanya biashara mkoani humo waliokuwa wakijishughulisha na
biashara mbalimbali zikiwemo za mafuta, sabuni, bati na nyinginezo huku
wakibainika kukwepa kulipa mapato ya serikali.
Aliendelea kusema
kuwa katika mamlaka hiyo aliitumikia zaidi ya miaka 11 akiwa ameitumikia
serikali kwa uaminifu hadi Februari, 1998 alipomwagiwa tindikali na
watu wasiojulikana wakati akigonga katika geti la nyumba aliyokuwa
akiishi eneo la Kirumba jijini Mwanza.
ANAIKUMBUKA SIKU HIYO YA BALAA
“Ilikuwa ni majira ya saa nne ya usiku nikiwa katika hali ya matembezi ya kawaida ambapo katika matembezi hayo walijitokeza baadhi ya wafanyabiashara ambao walinisalimia ndipo baada ya kuachana nao nilielekea nyumbani kwangu, nilipofika kwenye geti nilianza kugonga ili mlinzi aje afungue ghafla niliitwa jina langu na mtu niliyehisi alikuwa nyuma yangu, nilipogeuka, ghafla nilimwagiwa tindikali kichwani,” alisema Kombe.
“Ilikuwa ni majira ya saa nne ya usiku nikiwa katika hali ya matembezi ya kawaida ambapo katika matembezi hayo walijitokeza baadhi ya wafanyabiashara ambao walinisalimia ndipo baada ya kuachana nao nilielekea nyumbani kwangu, nilipofika kwenye geti nilianza kugonga ili mlinzi aje afungue ghafla niliitwa jina langu na mtu niliyehisi alikuwa nyuma yangu, nilipogeuka, ghafla nilimwagiwa tindikali kichwani,” alisema Kombe.
Akaongeza kuwa tukio hilo
lililoashiria kupangwa lilimletea maumivu makali ya kichwa ambapo
alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza na baadaye akahamishiwa
KCMC. Baada ya kushindikana katika hospitali hizo alipelekwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Leeds iliyopo nchini Uingereza kwa ajili ya
matibabu zaidi ambapo baada ya miezi minane alipata nafuu na kurudi
nchini.
Kombe ameshangazwa na hatua ya serikali kumlipa shilingi
milioni 12 kama mafao yake huku ikiwa imemtelekeza kwa kumwachisha kazi
wakati ana familia ya watoto wanne wanaomtegemea na kwamba fedha hizo
hazimtoshi kutokana na majeraha aliyoyapata katika eneo la kichwa na
maeneo mengine ya mwili wake.
“Naiomba serikali inipatie kazi kwani
ulemavu wangu hauwezi kunizuia kufanya kazi katika idara yoyote au
katika mamlaka hiyo hata kama ni kitengo cha huduma kwa wateja,
mawasiliano na nyinginezo ili niweze kujipatia kipato cha kuniwezesha
kuishi na familia yangu na kunisaidia katika matibabu.”
Yeyote
aliyeguswa na habari hii anaweza kumsaidia mpiganaji huyu wa uchumi wa
nchi hii kwa simu namba 0787 926549 Kutoa ni moyo.
No comments:
Post a Comment