Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa
Rukwa na Mpanda
wakimsindikiza kupanda ndege
msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania
Khadija Omar kopa kwenye uwanja wa
ndege wa mpanda baada ya
kupewa taarifa ya kufiwa
na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo alfajiri
kutokana na ugonjwa, Bi Khadija
Kopa alikua akitokea kwenye Maadhimisho ya
siku ya Mazingira Duniani kitaifa
yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.
Mkuu wa mkoa Rukwa Eng. Stalla Manyanya (kushoto)
akimfariji msanii wa taarab na malkia wa mipasho
Tanzania,Khadija omar Kopa alipokua kwenye chumba
maalum cha kupumzikia wageni kwenye
uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya
kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki
Dunia leo
Bi Khadija Kopa alikua kwenye maadhimisho ya
siku ya mazingira Duniani kitaifa
yaliyoaadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa juzi.