-Ni baada ya mtoto kugongwa na gari
-Barabara imefungwa kuanzia saa nne asubuhi
-Umati mkubwa wakusanyika eneo la tukio
KUNA vurugu zinaendelea eneo la Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam na wanachi wamefunga barabara baada ya mtoto kugongwa na lori na kupoteza maisha. Vurugu hizo zimeanza saa nne asubuhi baada ya ajali hiyo na mpaka sasa zinaendelea. Polisi wamefika eneo la tukio kujaribu kuzuia vurugu hizo lakini wameshindwa maana watu ni wengi. Kwa sasa hakuna gari lolote linalopita katika eneo hilo na baadhi ya wananchi wanachoma matairi. Habari zaidi, zitawajia baadaye
No comments:
Post a Comment