Abiria
hamsini na moja waliokuwa wakisafiri na basi la Taqwa kutoka Bujumbura
kuelekea Dar-es-Salaam wametekwa katika kijiji cha Milade wilayani
Mkalama na kuporwa mali , simu na fedha zaidi ya shilingi milioni mia
mbili hamsini.
Akieleza kamanda wa polisi mkoani Singida bwana Godfrey Kamwela amesema watekaji hao waliwaamrisha abiria kushuka chini ya basi baada ya kuvunja vyoo na kuanza kuwasachi na kufanikiwa kupora simu, fedha za kitanzania shilingi milioni tano ,dola za kimaerekani dola laki moja elfu sitini na faranga zenye thamani ya elfu ishirini kufuatia tukio hilo kamanda Kamwela amewaomba wananchi na makampuni ya simu kushirikiana na jeshi la polisi ili kuweza kuwa kamata watu ambao wamefanya tukio hilo
No comments:
Post a Comment