WASANII wanaotamba katika muziki wa Bongo Fleva, Kassim Mganga na Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ juzikati ilikuwa nusura wazichape baada ya kumwagiana matusi hadharani.
Rashid Makwilo ‘Chid Benz’.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni nje ya Ukumbi wa Bilicanas jijini
Dar baada ya Chid Benz kudaiwa kumrushia tuhuma Kassim kuwa ni mchawi
anayeroga wasanii wenzake.Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, Kassim alichukizwa na kauli hiyo na kumvaa Chid Benz huku akitoa matusi mazito na kuwataka watu waliokuwa karibu kuwaachia ili wachapane.
Kassim Mganga.
“Chid atawapiga wengine siyo miye,” alisikika akisema Kassim huku akirusha mashambulizi kwa kudai kuwa Chid anatumia ‘unga’.Hata hivyo, watu walioshuhudia tukio hilo waliwazuia wasipigane licha ya kwamba walishikana mashati huku kila mmoja akimrushia mwenzake maneno makali.
No comments:
Post a Comment