HABARI ambazo zilienea siku chache zilizopita za kwamba msanii wa filamu ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Endless Fame, Wema Sepetu amekamatwa nchini China kwa soo la unga’ na kuripotiwa na gazeti moja la wiki (siyo la Global) zimeonesha kumuumiza sana mlimbwende huyo na kuamua kufunguka.
Akichati na Ijumaa juzi kupitia mtandao wa Instagram Wema alisema: “Siwezi kusema niko na furaha kabisa. Nimesema niondoke zangu Bongo kimyakimya kuja huku kuhangaikia kazi zangu, nimeonekana nimekuja kuuza unga.
“Maskini ya Mungu naishi maisha yangu wala sina habari na mtu, sijawahi hata siku moja kufikiria kufanya biashara hiyo, leo nimelia na naumia sana.”
Madai ya Wema kunaswa China kwa soo la ‘poda’ yamekuja ikiwa ni siku chache tu tangu Video Queen, Rehema Fabian akiri kutupwa selo nchini humo kwa kesi ya madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment