kaa tayari kwa blog yangu mpya ya fashion JACK255.BLOGSPOT.COM....

SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG

Monday, 30 September 2013

Miss Philippines ndio ameibuka mshindi wa Miss World 2013

Miss kutoka Philippines Megan Young ndio amevishwa taji la Miss World 2013 iliyofanyika usiku wa jumamosi, Bali Nusa Dua Convention Center Indonesia.

"I promise to be the best Miss World ever," Alisema Miss Megan baada ya kuvishwa taji hilo na miss world 2012, Wenxia Yu.

Young, ambae alizaliwa nchini Marekani amewashinda wasichana wengine 126 walioshiriki katika shindano hili ambalo ni la 63 tangu kuanzishwa.

Megan alihamia Philippines alipokuwa na miaka 10 na amekuwa akiishi huko mpaka hivi sasa, na kufanya kazi kama muigizaji na mtangazaji wa Televishen.

Miss France, Marine Lorphelin, 20, amekamata nafasi ya pili na Miss Ghana Carranzar Naa Okailey amekuwa wa tatu.

Miss Tanzania alieshiriki shindano hilo mwaka huu, Brigitte Alfred, ameibuka nafasi ya tatu katika shindano la Beauty with a purpose ikiwa ni shindano linaloenda sambamba na shindano la Miss World

No comments: