Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya
amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake
chooni. Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza
kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo.
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
Ameongeza
kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo
tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
Rukia
Haruna (31) akitolewa nje na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje
ya Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela
Mwendesha
Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya
Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia
Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume
cha kifungu 218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.
No comments:
Post a Comment