Ikiwa ni siku chache baada ya wasanii kuahirisha show zao
kufuatia kuondokewa mpendwa wetu Albert Mangwea, miongoni mwa show kubwa
zilizoahirishwa ni ya Lady Jay Dee (Miaka 13 ya Lady JayDee) na ya Mwana FA
(The Finest) zilizokuwa zifanyike siku moja (May 31),show hizi zinaweza
kufanyika tena siku moja kwa kuwa wasanii hao wametaja tarehe inayofanana.
May 28 ambayo ndiyo siku aliyofariki Mangwea mwana FA
alithibitisha kuahirisha show yake, lakini alipoulizwa siku ambayo anadhani
atairudia show hiyo, yeye alifunguka kupitia akaunti yake ya twitter na kuitaja
June 14.
“Sina uhakika,but
I'll pick June 14th kama brother tutakuwa tushampumzisha"@umykitwana”,
alitweet Mwana FA a.k.a Binamu.
Kwa upande wake Lady Jay Dee ambae kwa sasa a.k.a yake mpya
‘Anaconda’ inaonekana ku-take over ametumia akaunti yake ya twitter kuiweka
wazi tarehe ya show yake alipokua akijibu swali la fan wake ambae atasherehekea
siku moja ya kuzaliwa na msanii huyo (June 15).
“@MteiHaikaJ Gud. Chukua hii tar 13 June Mahakamani, tar 14
June miaka 13 ya Jide na tar 15 June Bday ya Jide. Let's celebrate long week
end.”Alitweet Lady Jay Dee June 2.
Kwa tweets za wakali hawa wa bongo fleva inaonesha kabisa
kuwa show zao zinaweza kufanyika june 14 japo Mwana FA alisema hana uhakika,
labda kama atatangaza siku nyingine tena. June 14,tunatarajia kuwa marehemu
Ngwair atakuwa amekwisha pumzishwa kwenye nyumba yake ya milele huko Morogoro.
CHANZO : LEOTAINMENT