Baada ya
watanzania wengi na wadau wa muziki kujiuliza kuhusu hatma ya malipo ya nyimbo
za marehemu Albert Mangwea zilizokuwa zikitumika katika miiito ya simu, maswali
hayo yamepatiwa majibu na kampuni ya Push inayohusika na zoezi zima la kuuza
miito ya simu (CBRT).
Kampuni hiyo
imetoa tamko rasmi na kuwahimiza watanzania na wapenzi wa Ngwea kuendelea
kununua kwa wingi nyimbo zake kama miito ya simu kwa kuwa malipo yake yanaendelea
kusimamiwa na Bongo Records ambao ndio wasambazaji wa kazi za Marehemu.