kaa tayari kwa blog yangu mpya ya fashion JACK255.BLOGSPOT.COM....

SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG

Tuesday 23 April 2013

AVRIL KUZINDUA SINGLE YAKE NA OMMY DIMPOZ TAREHE 30 APRIL


Siku ya mkesha wa kuamkia sikukuu ya wafanyakazi "mei mosi", Msanii kutoka Kenya Avril anatarajia kuzindua single yake aliyomshirikisha Ommy Dimpoz huku perfomace za wasanii kutoka Kenya na Bongo zikitawala 

185 WAUAWA KATIKA MAPIGANO NIGERIA-bbc swahili news


Wapiganaji wa kundi wa Kiislamu la Boko Haramu


Zaidi ya raiya mia moja na themanini na tano wamefariki huku nyumba elfu mbili zikiharibiwa kutokana na mapigano makali kati ya jeshi na wapiganaji wa Kiislamu kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Serikali ya mji wa Baga na Ofisa Serikali hiyo Bwana Lawan Kole
Jeshi na maafisa wa serikali wanasema kuwa kulikuwa na mashambulizi ya gurunedi, zilizosukumwa na roketi na makabiliano ya risasi katika mji tulivu wa Baga unaopakana na Chard Ijumaa jioni.
Wakazi walikimbili misituni na kurejea hapo jana ila walipata sehemu kubwa ya mji huo imeharibiwa na maiti na mizoga ikiwa imetapakaa kila mahali.
Mwanahabari mmoja amesema kuwa hali hiyo inadhirisha namna mapigano yamezidi Nigeria katika eneo la Kasikazini ambalo lina waislamu wengi.
Alisema wapiganaji walikuwa na silaha nzito kuliko zilizotumika katika mashambulizi ya hapo awali katika eneo hilo nao manusura wanasema washambuliaji wengi walikuwa wakizungumza lugha ya kigeni.
Inasemekana kuwa watu wengi zaidi wamefariki dunia ambapo bado juhudi za kutafuta maiti nyingine zinaendelea.
Brigedia Jenarali Austin Edokpaye amewaambia maafisa wakuu wa serikali kuwa,wapiganaji walitumia silaha kali na maroketi yenye mabomu mazito kupambana na vikosi vya jeshi.
Aidha bwana Edokpaye aliongeza kuwa,wapiganaji hao walikuwa wakitumia raia kama kinga yao kwa kujibanza karibu na makaazi ya watu ambapo walijua vikosi vya jeshi visingeweza kujibu mapigo.
Nigeria imekuwa ikikabiliwa na vifo vya raia wengi tangu kuibuka kwa vikundi vya wapiganaji wa kiislamu mwaka 2010 ambapo vingi vimejikita Kaskazini mwa nchi hiyo.




DIAMOND NDANI YA LONDON MWEZI HUU

OUR OWN FINEST MODEL: MILLEN MAGESE SPOTTED IN KITENGE


KUTOKA ACCOUNT YA MWANAMITINDO MILLEN MAGESE

THIS MIGHT BE YOUR WEEKEND LOOK (MEN):suggested by pincode designer

H.BABA AINGIZA SOKONI PIPI MPYA ZENYE JINA LA JINA LAKE NA MKEWE


PICHA YA LEO