![](http://api.ning.com/files/7Yks3h911A-kyEK7qVGswy3YOOcRDsCGH92AiYJGQr*LKWNeO1WfCat5mODYjuS0QCCYrttxShuE5Onf-vSv5Od86G6fjQid/KICHAPO.jpg?width=650)
WAKATI Oparesheni Fichua Maovu (OFM) inayoendeshwa na Global Publishers ikiwa mzigoni, imenasa tukio la fedheha kwa njemba mmoja akichezea kichapo ‘hevi’ kutoka kwa wanawake waliosadikiwa kuwa machangudoa.
![](http://api.ning.com/files/7Yks3h911A9wlhMOQXfh2pX4za1GQxW2g9MHqkY-VWkHaza0aYtid0cVfP6q8c4YEsT-r9ud84R1l9ALJ-x831BC32CeqV21/KICHAPO3.jpg?width=450)
Mashuhuda wa tukio hilo ambao kwa sehemu kubwa walikuwa ni madada poa, walidai kuwa baada ya jamaa huyo kupewa huduma ya penzi jirani na eneo hilo aligoma kulipa hivyo timbwili zito likaibuka.
![](http://api.ning.com/files/7Yks3h911A-W6UtiAZ9KOxAJf7OvZBdsM11jxctIRAy9hbQcW3CQIUHSPM5ApQMiXOSPiD7u-4VHgcxtN521Lvl6Kg5aUg7A/KICHAPO2.jpg?width=450)
Pamoja na kufurukuta, jamaa huyo alishindwa kuhimili mangumi ya wanawake hao waliokuwa na hasira ya ajabu hadi akajikuta akitokwa na kijasho chembamba kabla ya kufanikiwa kuwakimbia.
![](http://api.ning.com/files/7Yks3h911A9H1VXT*kxHy18QGilN3qAuyQn*NdWyVSS3e9HRr4*S2RgRFyXTKSpf**45BaLa7dOLzXdO8akucNALLS8cHNYz/KICHAPO1.jpg?width=450)
“Haiwezekani mtu tumekubaliana vizuri na amepata huduma safi, iweje agome kutoa mtonyo (fedha)? Hii ni kazi kama kazi nyingine kwa nini asiiheshimu? Anadhani mimi nitakula wapi wakati ajira zenyewe wanapeana wakubwa?” alihoji mwanamke huyo huku akiondoka eneo hilo baada ya kutulizwa mizuka na wenzake.