SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG
Thursday, 3 October 2013
DIAMOND PLATINUMZ AKABIDHI iPAD KWA MSHINDI WA NGOLOLO
Licha ya kuvuja kwenye internet, album ya Drake imeshika namba moja kwenye chart ya Billbord Top 200
![drake-happy-sad-new-650](http://millardayo.com/wp-content/uploads/2013/10/drake-happy-sad-new-650.jpg)
Licha ya kuvuja kwenye mtandao wiki moja kabla ya tarehe rasmi ya kutoka, album ya Drake Nothing wa The Same imeshika namba moja kwenye wiki yake ya kwanza tangu itoke na imekua album ya pili kwa kufanya mauzo mazuri kwa album zote zilizotoka kwenye wiki hii. Mafanikio mengine ambayo album ya “Nothing was the same” imepata ni kuyapita mauzo ya album za zamani kutoka kwa Drake.
Ndani ya wiki ya kwanza album yake ya “Take Care,” iliuza nakala 631,000, “Thank Me Later,”iliuza 447,000 , “So Far Gone,” iliuza nakala 73,000. Nothing was the same imeuza nakala 658,000 katika wiki ya kwanza na kuvunja rekodi ya album zake zilizopita.
Drake alifanyiwa interview na ex-girlfriend kwenye show ya 106&Park ikiwa ni moja ya promotion za album yake mopya. Drake alikuwa na mahusiano na binti huyu enzi hizo wakiwa Canada na hivi sasa ni mtangazaji mpya kwenye show hii ya BET
DUDE ABAMBWA AKIWA NA KIDOSHO
![](http://api.ning.com/files/2QN5aCZBKSYQVpqYdzQ98QR-mmM9eNNk5NV1*9YczOXZTkrpiejlAuzcPcxI2QPm80G6hjKvla9UjK2QOps4VK9JVqgMDukO/dude.jpg?width=650)
STAA wa sinema za Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ juzikati alinaswa na kamera ya Amani akiwa na kidosho ndani ya gari tayari kwa kwenda kusikojulikana.
Dude alikutwa akiwa na ‘mzigo’ huo Mlimani City, jijini Dar ambapo mastaa wengi huenda eneo hilo kujiachia. Kidosho huyo alijulikana kwa jina moja la Fetty.
“We vipi na hiyo kamera yako kwani kuna kosa gani mi’ kupanda gari moja na Dude? Nioneshe sheria ambayo hairuhusu mwanamke na mwanaume kuwa katika gari moja, isitoshe Dude ni ‘director’ (mwongozaji sinema) wangu katika filamu ninayoindaa,” alifululiza kusema mrembo huyo wakati wanaondoka.
Ulimiss kuisoma barua aliyoandikiwa Shilole na mwanae?, basi isome hapa
![SHILOLE](http://millardayo.com/wp-content/uploads/2013/10/SHILOLE.jpg)
“I miss you so much mom and I love so much you mother. Since I go to school I was worried about”, haya ni baadhi ya maneno ambayo ameandika mtoto wake Shilole.Bila kujali kupatia au kukosea kuandika kwa lugha aliyotumia, kitu kikubwa ni mapenzi kati ya mama na mwanae. Barua hii aliandika mtoto wa Shilole kumuachia mama yake nyumbani. Shilole anasema aliikuta hii barua alivyorudi kutoka Fiesta Mwanza na mwanae akiwa ameenda Shuleni. Cheki picha ya barua yenyewe na usisome yote hapa
![SHILOLE2](http://millardayo.com/wp-content/uploads/2013/10/SHILOLE2.jpg)
WEMA, DIAMOND WARUDIANA
![](http://api.ning.com/files/2QN5aCZBKSZS7BCte8mCL00M*nGxK03ujKutPbUBEykWT*RAGGXIZ3US89ZLFkxLd65hA3g7y5k5ehd44OAUHzWXrlfp7zOk/diomond.jpg?width=650)
WACHUMBA wa zamani, Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ ndiyo habari ya mjini kwa sasa, kwamba wawili hao wamerudiana tena kwa kasi kupita ile ya mwanzo, Amani limechimbua.
Habari zinasema wawili hao walikutana Dubai
hivi karibuni kabla Diamond hajaenda Malaysia na Wema akiwa njiani
kuelekea Hong Kong, China ambapo walikula bata kwa sana.
Ikazidi kuelezwa kuwa wameamua kuwa kwenye uhusiano wa siri na lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha mpenzi wa sasa wa msanii huyo wa Bongo Fleva, Penniel Mungilwa ‘Penny’ hajui kitu chochote.
TAARIFA ILIVYO
Kwa muda wa siku nne, ndani ya mitandao ya kijamii hasa kwenye Instagram, maneno yenye kuashiria kuwa wawili hao wapo pamoja tena yamekuwa yakichukua nafasi.
Baada ya kusambaa kwa habari hizo, Penny naye alitupia picha yake akiwa kitandani na Diamond na kuandika kuwa waachwe kama walivyo.
Ndani ya mtandao wa Instagram yakazuka makundi mawili, upande wa mawifi wa Penny, akiwemo Halima Kimwana na kundi lingine la mawifi wa upande wa Wema.
Kundi la Wema waliandika kuwa mwanamke anayependwa na ndugu wa mume siku zote mwanamme huwa hampendi hivyo Wema ni mpenzi sahihi wa Diamond kwa vile hapendwi na ndugu kama Penny.

MBAYA ZAIDI
Mbaya zaidi, katika hali isiyotegemewa kwenye akaunti yake ya Instagram, Wema alitupia wimbo mpya wa Diamond uitwao My Number One na kuweka maoni yake kwamba anaupenda wimbo huo.
Wengine waliochangia walisema Wema ana lake jambo kwa Penny kwa vile si jambo jepesi kusifia wimbo wa mwanamme ambaye alikuwa mpenzi wake na sasa ana mwingine anayejulikana, yaani Penny.
PICHA YA WEMA SASA
Wema hakuishia kuposti wimbo huo tu, alikwenda mbele zaidi kwa kutupia picha yake yenye pozi tamu na kuuliza; huyu hapa baby wa nani huyu? (yaani yeye).
Wengi walimsifia lakini wengine walifunguka kwa kusema ni baby wa Diamond, jambo ambalo Wema hakulipinga.
PENNY AONGEA NA AMANIMbaya zaidi, katika hali isiyotegemewa kwenye akaunti yake ya Instagram, Wema alitupia wimbo mpya wa Diamond uitwao My Number One na kuweka maoni yake kwamba anaupenda wimbo huo.
Wengine waliochangia walisema Wema ana lake jambo kwa Penny kwa vile si jambo jepesi kusifia wimbo wa mwanamme ambaye alikuwa mpenzi wake na sasa ana mwingine anayejulikana, yaani Penny.
PICHA YA WEMA SASA
Wema hakuishia kuposti wimbo huo tu, alikwenda mbele zaidi kwa kutupia picha yake yenye pozi tamu na kuuliza; huyu hapa baby wa nani huyu? (yaani yeye).
Wengi walimsifia lakini wengine walifunguka kwa kusema ni baby wa Diamond, jambo ambalo Wema hakulipinga.
Kufuatia kuenea kwa habari hizo, Amani lilianza kuwasaka watu watatu ambao ndiyo wenye uwezo wa kubainisha ukweli au uongo wa ishu hiyo iliyoenea mjini.
Watu hao ni Diamond mwenyewe, Wema anayedaiwa kurudiwa na Penny, mpenzi wa sasa wa Diamond.
Wa kwanza kupatikana alikuwa Penny ambapo alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa madai hayo alifunguka:
AKIRI KUNYETISHIWA
“Ni kweli hata mimi nimenyetishiwa habari hizo lakini siamini kama inawezekana hao watu wakarudiana.
ASEMA KUNA KUNDI LINAPANGA NJAMA
“Nijuavyo mimi kuna kundi la watu ambao wapo upande wa pili (wa Wema) ndiyo wanaoeneza hizo habari, pengine wanataka niamini kisha nimwache Diamond, simuachi ng’o.
ANATAKA USHAHIDI WA PICHA
“Kama niliweza kumvumilia kwa kuona picha akiwa na Irene Uwoya hotelini sembuse hili la safari hii hata picha hakuna?”
ALISHAMUULIZA DIAMOND
“Mimi nilishamuuliza Diamond, japo hakusema ni kweli au uongo ila aliniambia achana na hizo habari.”
DIAMOND APIGA KIMYA
Baada ya kuongea na Penny,
lilimpigia simu Diamond ambapo alipokea na kusema yuko kikaoni na kumtaka paparazi kupiga baadaye. Hiyo ilikuwa saa 4:16 asubuhi ya juzi.
Saa 7:11 mchana, Diamond alipigiwa simu tena lakini hakupokea. Akatumiwa meseji ya kumkumbushia, hakujibu. Akatumiwa meseji yenye madai ambayo pia hakuijibu.
MAMA WEMA KABLA YA KUULIZWA AFUNGUKIA MADAWA YA KULEVYA
Amani liligundua Wema bado yupo Hong Kong hivyo liliamua kumpigia simu mama yake, Bi. Miriam Sepetu ili kuomba namba ya bintiye, lakini kabla ya ombi hali ikawa hivi:
“We nani, hivi kuna gazeti moja limeandika eti mwanangu amekamatwa na madawa ya kulevya China anasubiri kunyongwa, ni akina nani wale, wana akili kweli?
“Mimi sikubali safari hii, tutafikishana kwa mwanasheria wangu.
“Tena ukikutana nao waambie waache kumzushia mwanangu, wasimtie mkosi bure, hajakamatwa yupo salama kabisa.”
Mpaka sasa ushahidi wa kuonesha wapenzi hao wa zamani kuwa wamerudiana bado haujawekwa hadharani.
Imeandikwa na: Shakoor Jongo, Hamida Hassan, Gladness Mallya na Imelda Mtema.
MAJAMBAZI YATEKA BASI LA ABIRIA NA KUPORA SIMU NA FEDHA.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhjskzYSdiKfFT7aMWKXjOnuGujZWYdi1BAgINM6w_tpAmrQdUia6uN72_A0V1yZh6gmBd7ldL8Ym5-tCra96pvB1Myy_oxZEn2HwbCm2dShQZLwIHG7x45-CG-mcyyDYLaafYUG3tDUs58/s640/aa1.webp)
Abiria
hamsini na moja waliokuwa wakisafiri na basi la Taqwa kutoka Bujumbura
kuelekea Dar-es-Salaam wametekwa katika kijiji cha Milade wilayani
Mkalama na kuporwa mali , simu na fedha zaidi ya shilingi milioni mia
mbili hamsini.
Akieleza kamanda wa polisi mkoani Singida bwana Godfrey Kamwela amesema watekaji hao waliwaamrisha abiria kushuka chini ya basi baada ya kuvunja vyoo na kuanza kuwasachi na kufanikiwa kupora simu, fedha za kitanzania shilingi milioni tano ,dola za kimaerekani dola laki moja elfu sitini na faranga zenye thamani ya elfu ishirini kufuatia tukio hilo kamanda Kamwela amewaomba wananchi na makampuni ya simu kushirikiana na jeshi la polisi ili kuweza kuwa kamata watu ambao wamefanya tukio hilo
MAMA - NITAMNYONYESHA MWANANGU KWA MIAKA 10 KAMA AKITAKA
MWANAMKE mmoja wa New South Wales, nchini Australia, aitwaye Maha Al
Musa, amekuwa akimnyonyesha mwanaye ambaye sasa ana umri wa miaka
mitano.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 51 ambaye ni msanii wa burudani ya unenguaji, aliacha kuwanyonyesha watoto wake wawili hadi walipofikia miaka miwili kila mmoja, lakini mwanaye wa sasa ambaye ni wa tatu, ameamua kuendelea kumnyonyesha kwa vile alihisi alikuwa ‘amebarikiwa’ na ameahidi kwamba ataendelea kumnyonyesha hadi afikie umri wa miaka kumi iwapo atataka kuendelea kunyonya.
Maha aliwaachisha watoto wake wawili -- Kailash ambaye sasa ana miaka 16, na Tariq, (13), wakiwa na miaka miwili kila mmoja.
Al Musa amefuata nyayo za Jamie Lynne Grumet (26) wa Los Angeles, Marekani, ambaye aliwashangaza watu baada ya kutolewa na jarida la Time lililomwonyesha akimnyonyesha mtoto wake wa miaka minne.
Wakati mtoto wake Al Musa amefikisha miaka mitano, mama huyo anasema hajali wanachosema watu kuhusu jambo hilo
“Ninaamini kuendelea kwake kunyonya kunamjengea kinga dhidi ya magonjwa kwani yuko katika afya njema na utulivu kuliko watoto wengine,” anasema mama huyo.
Naye Grumet ambaye alinyonyeshwa na mama yake hadi kufikia umri wa miaka sita na aliyekuwa akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni, aliunga mkono unyonyeshaji wa namna hiyo, japokua watu hushangaa.

OMMY DIMPOZ ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg16d0_ywdJuwA4K2Zoi9Sggkt8biQUy4NM29H0RO9fasj1CDPKGpce8GpNDLy6S8OABCWSYv-K09NijBiUQX3M1AW6E6cDVGk8kUIcCh9SYCstLEBKFzsLwX2kGmfQ9SGkZbsk62FQT6k/s640/20131002_131509.jpg?width=640)
Mwanamuziki Ommy Dimpoz akitia saini katika kitabu cha wageni ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington DC.…
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg16d0_ywdJuwA4K2Zoi9Sggkt8biQUy4NM29H0RO9fasj1CDPKGpce8GpNDLy6S8OABCWSYv-K09NijBiUQX3M1AW6E6cDVGk8kUIcCh9SYCstLEBKFzsLwX2kGmfQ9SGkZbsk62FQT6k/s640/20131002_131509.jpg?width=640)
Ommy
Dimpoz akiwa na Balozi Mulamula (katikati) na Promota wake DMK ambaye
pia ni Mkurugenzi wa MMK Media Group kampuni inayomiliki Swahili Radio
Online, Swahili TV Online, Swahilitv Blog na DMK411 Blog.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhgUYJyqmq4T2fdQEAnEgRpAj3zqGSwTzkWTmHWJPlLRDgV5xK72dAKKgC3XyznGrRWyfn-Q59Rzu_O2Pu6Q5RDk8ern-EKkr1xO3eLrX1RuEhYjvByLWIClGeaikdxC7P1IHavewQ05fk/s640/20131002_142249.jpg)

Mheshimiwa Balozi katika pozi na Poz kwa Poz.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA SWAHILITV BLOG
BREAKING NEWS: VURUGU ZATOKEA MBAGALA, BARABARA YAFUNGWA
![](http://api.ning.com/files/2QN5aCZBKSbYVKJLlobpTB7lnr90oZtolBIR*z5WB*xpZ9U9N02oVKbxP52oyvSohI7gSSvQxkbvReMXsIpDDquRczOIxPxr/BREAKINGNEWS.gif)
-Ni baada ya mtoto kugongwa na gari
-Barabara imefungwa kuanzia saa nne asubuhi
-Umati mkubwa wakusanyika eneo la tukio
KUNA vurugu zinaendelea eneo la Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam na wanachi wamefunga barabara baada ya mtoto kugongwa na lori na kupoteza maisha. Vurugu hizo zimeanza saa nne asubuhi baada ya ajali hiyo na mpaka sasa zinaendelea. Polisi wamefika eneo la tukio kujaribu kuzuia vurugu hizo lakini wameshindwa maana watu ni wengi. Kwa sasa hakuna gari lolote linalopita katika eneo hilo na baadhi ya wananchi wanachoma matairi. Habari zaidi, zitawajia baadaye
PICHA: TRENI YA MWAKYEMBE ILIVYOGONGWA NA LORI LA MIZIGO ENEO LA BUGURUNI BAKHERESA.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj8xgH_EMVtkWsoyDOSlvI62eZRPi7SlhcEMqNujeEN4mQu2iO3ChA25lscT6AYjnxVcKySaGJTx2QGGmLbCrVicBB74wpeZdQn55Hkw0tr8si6jpAg0ALcS3L0xeUELaf1hzRQ2VVucOg/s640/IMG-20131002-WA0019.jpg)
Lori lililogonga treni ya Mwakyembe lililokuwa likitoka Stesheni kuelekea ubungo kwenye majira ya Saa kumi na Mbili Jioni ya leo Likiwa limepinduka mara baada ya kuligonga treni hilo eneo la Buguruni Bakheresa
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi0VXLKd_47wrQG1Nlq4z2kFHWDueeGWW_zTgMmKFVosDUnAYJYtOWdTM99E3VA4OTVpb0q0wmudr9goJWeM06b4tQbUltT0VPHYJqSW6BtbaOPngUo5Sl3PM6kA40nOwOeHO7RNJbEU48/s640/IMG-20131002-WA0003.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgXlbuwuEiiDWsb5HBWoDIOAvf96as_V_aCvufAMomUUFUjJnmdEVEBk8oXJvb4XcfEA1VBR-Di2AD6-YM0EY76hBaVCJ9N68_EtHQIVlvsklTp7D2vT8IK9OqUVNXsbOJuLtlag3A48Iw/s640/IMG-20131002-WA0004.jpg)
Wakazi wa jiji la Dar na Wapita njia wakishangaa lori lililogonga treni ya Mwakyembe iliyokuwa ikitoka Stesheni kuelekea Ubungo majira ya Saa Kumi jioni ya leo(jana)
Subscribe to:
Posts (Atom)