kaa tayari kwa blog yangu mpya ya fashion JACK255.BLOGSPOT.COM....

SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG

Friday 27 September 2013

MAMA AMKATAA MTOTO WA SHARO MILIONEA


Stori: Hamida haasan na Gladness Mallya
MAMA wa aliyekuwa msanii maarufu Bongo, marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Millionea’, Zainab Mkiety amemkataa mtoto ambaye alipelekewa Tanga na mama yake anayetokea Geita akidai ni damu ya Sharo.

Mtu wa karibu na familia hiyo ameliambia gazeti hili kuwa baada ya msiba kupoa, mama wa mtoto huyo alifunga virago na mwanaye kwa ajili ya kwenda kutembelea kaburi la Sharo na kwenda kujitambulisha kwa bibi wa mtoto.
Chanzo hicho kilieleza kuwa mama mtoto huyo alipofika Muheza jijini Tanga, alipokelewa na watu wa bodaboda ambao walimsindikiza hadi nyumbani kwa mama Sharo.
“Alipofika alipokelewa lakini cha kushangaza mama Sharo alimkataa na kusema marehemu hakuwa na mtoto kwa sababu hakuwahi kumwambia,” alisema sosi huyo.

Ili kupata ukweli wa habari hiyo, paparazi wetu aliwasiliana na mama Sharo kwa simu ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli alikuja mwanamke akiwa amebeba mtoto ambaye alijitambulisha kwangu kuwa ametokea Geita.
“Alisema mtoto aliyekuwa amembeba ni wa Sharo lakini nilikataa nikamwambia kuwa mwanangu hakuwahi kuniambia kuwa ana mtoto na nilipowauliza marafiki zake walisema hawana taarifa hizo.
Nisingeweza kumpokea kwa sababu alishajitokeza mwingine na kudai kuwa ana mimba ya mwanangu, baada ya kumkataa mwanamke huyo aliondoka na mpaka leo sina mawasiliano naye.”
Sharo alifariki dunia kwa ajali ya gari Novemba 26, mwaka jana katika Kijiji cha Maguzoni-Soga, Wilaya ya Muheza jijini Tanga.

HIVI NDIVYO JENGO LA WESTGATE LILIVYOPOROMOKA BAADA YA MLIPUKO HUKO KENYA....!!

Kupomomoka kwa jengo la ghorofa tatu ndani ya Westgate Mall baada ya mlipuko uliosababisha vifo vya magaidi wa 5 na na wengine 11 kushikiliwa na Polisi siku ya Jumamtatu Sept 23, 2013 kama unavyoonekana katika picha magari yaliyokua yameegeshwa juu ya paa la magesho ya magari yakiwa yameanguka chini kwa mlipuko huo. Westgate

Conflicting reports: A minister said the terrorists had set mattresses on fire, causing the roof to collapse

Paa la maegesho ya magari likiwa limebomoka kutokana na mlipuko huo.

Assessing the damage: Kenyan government officials accompanied by armed security officers tour an outside upper level near a collapsed floor of the Westgate mall

Wananusalama wakijadili jambo baada ya jaribio hilo la Westgate Mall kuzimwa baada ya mlipuko uliosababisha jengo la ghorofa 3 kuporomoka baada ya magaidi wa Al Shabab kuvamia Mall hiyo siku ya Jumamosi Sept 21, 2013 na kusababisha vifo nya watu 69 na wengine 175 kujeruhiwa huku kikundi hicho cha Kigaidi kudai kwamba hawataishia hapo mpaka Kenya itakapoondoa majeshi yake Somalia.

HIYU NDO MSANII WA BONGO MOVIE ALIYEZOMEWA BAADA YA KUKATIZA MTAANI NA NGUO YA NUSU UTUPU

MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Tamrina Posh ‘Amanda’ amejikuta katika wakati mgumu wa kuzomewa kutokana na kukatiza kitaa akiwa na nguo iliyombana na kuonesha makalio yake yaliyojazia.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, tukio hilo lilichukua nafasi Ijumaa iliyopita maeneo ya Mwenge, jijini Dar ambapo msanii huyo alikuwa ameenda kwa ajili ya kununua mahitaji mbalimbali ndipo kundi la wanaume wakware lilipoanza kumzomea.

Tukio hilo lilimfanya Amanda apoteze amani ghafla na kuamua kutimka zake eneo hilo huku akiwashangaa. Paparazi wetu hakuwa nyuma, alimpigia simu na kumuuliza kulikoni?

“Daah! Ilikuwa kero kweli, wanaume wazima wanaacha kazi zao na kuanza kunizomea huku wakiniambia kuwa ni dawa za Kichina. Lakini ukweli ni kuwa hii ni asili yangu na si Mchina,” alisema Amanda.

TABIA YA KUTOVAA NGUO ZA NDANI YAMTOKEA PUANI MSANII TIWA SAVAGE,KILA KITU CHAANIKWA HADHARANI


Msanii  huyu   toka  Nigeria amejikuta  akiambulia  aibu  baada  ya  nyeti  zake  kuanikwa  hadharani  wakati  akitumbuiza  jukwaani...

Tiwa  alikuwa  akitumbuiza  jukwaani huku  akiwa  na  kisiketi  kifupi ambacho  kilianika  kila  kitu  kwa  kuwa  ndani  hakuvaa  KUFULI...


Kilichomstua  ni  baada  ya kuona  watu  wako  bize  na  simu  zao  wakipiga  picha  hasa  eneo  la  chini  alipokuwa  amesimama  juu ya  jukwaa...


Hali  hiyo  ilimfanya  akatishe  show  kwa  muda ili  kupata  muda  wa  kujiweka  vizuri.

( THE WORLD'S LARGEST TORTOISE) -AMINI USIAMINI HUYU NDO KOBE MKUBWA KULIKO WOTE ANA..MIAKA 529


The World’s largest tortoise found in Amazon River is around 529 years old / height-59 feet/ weight-800 pounds OR 362.87 kg incredible.

The red rimmed tortoise is also called the red-foot or red-legged tortoise, the Brazilian giant tortoise, or South American forest tortoise.

These types of large size tortoise are always found in the Amazon River, most of them are found in (Peru, Brazil, Colombia, Venezuela, and so on) the Adults often reach 3m in length, however this one is much larger. The tortoise Females have wide flattened shells, are larger and more numerous than the males tortoise, the Adult tortoise Arraus feed entirely on plant food.

Their main diet is a plant that is native to the Chtac Province region of Brazil. These flowers of this plant have a gene in them which promotes increased cellular life thus allowing those that consumed them to have a greater lifespan. Amongst the native inhabitants are turtle’s that grew constantly in their lifespan until the day they died. The introduction of this flower into their diet thus allowed them to grow to immense sizes and they served as local guardians to the plant.

It was first discovered by the modern world in 1892 by Haughton who was the last person to had seen it in the century.

The nesting habits of this species are similar to those of sea turtles. Just like sea turtles they gather meet in huge numbers so they can travel to suitable nesting areas. The female tortoise lay their eggs on sandbanks that are exposed where there is only dry season but there are relatively few such sites.

MRISHO NGASA NOMA AWAONYESHA TFF JEURI YA FEDHA

Na Ezekiel Kitula
MSHAMBULIAJI Mrisho Ngassa wa Yanga, ameuambia uongozi wake yupo tayari ulilipe Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kitita cha Sh milioni 45 kutoka kwenye mshahara wake.
Ngassa amekubali kitita hicho cha fedha kitolewe kwa kuwa ana hamu ya kuanza kuitumikia Yanga baada ya kumaliza adhabu ya kutocheza mechi sita aliyopewa na TFF.
Imeelezwa Ngassa yupo tayari kukatwa katika mshahara wake na kuna taarifa katika Sh milioni 2 kila mwezi, atakatwa Sh 500,000.
Mshambuliaji huyo alisimamishwa mechi sita pamoja na kutakiwa kurudisha Sh milioni 30 alizolipwa na Simba pamoja na faini ya Sh milioni 15. TFF ilishikilia msimamo wake kwamba Ngassa hatacheza hadi atakapolipa fedha hizo za Simba.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa, Ngassa amekubali kuhusiana na hilo na alifikia makubaliano hayo na mwenyekiti, Yusuf Manji walipofanya kikao walipokutana jijini Mbeya, hivi karibuni.
Alipoulizwa kuhusiana na hilo jana, Ngassa alisema:  “Sawa, adhabu yangu ya kutocheza mechi sita za mashindano imemalizika, lakini siwezi kuongelea lolote, mimi ni mchezaji tu, kazi yangu ni ndani ya uwanja, hayo mengine ya kiutawala ni vyema yakatolewa ufafanuzi na viongozi,” alisema Ngassa.
Championi Jumatano lilimtafuta Manji ambaye alikiri kuzungumza na Ngassa kuhusiana na masuala kadhaa ya klabu yao likiwemo hilo.
“Mimi ni mwenyekiti, hakuna ubaya kuzungumza na Ngassa. Tunazungumza kwa ajili ya klabu yetu, hivyo msubiri akicheza mtamuona,” alisema Manji.
Taarifa nyingine zilieleza kuwa, Yanga ilikuwa tayari kupeleka fedha hizo leo, lakini ilitaka TFF wakate Sh milioni 45 katika Sh milioni 70 inazowadai na walikuwa katika mazungumzo katika hilo.
Kwa upande mwingine, Kocha Mkuu, Ernie Brandts, alisisitiza kwamba ana kila sababu ya kumpanga Ngassa kama atakuwa amerejea katika kikosi watakapoivaa Ruvu Shooting Jumamosi.
“Tuko naye kikosini kila siku, tunafanya naye mazoezi na tunashirikiana. Kama amerejea na yuko katika afya nzuri, nitampanga maana ninamhitaji,” alisema Brandts.
Wakati hilo la Ngassa linamalizika, taarifa nyingine za uhakika zimeeleza Manji alitarajia kukutana na kikosi kizima cha Yanga, jana usiku.
Mwenyekiti huyo alipanga kukutana na wachezaji na benchi la ufundi katika hoteli ya Serena jijini Dar ili kula chakula cha usiku na baadaye kujadili masuala kadhaa kikiwemo kipigo cha Azam FC na nini cha kufanya baada ya hapo ili kusonga mbele na ikiwezekana kutetea

AGNESS MASOGANGE AAHIDIWA NDOA MARA ATAKAPOTUA BONGO...!!


MCHUMBA wa ‘video queen’ maarufu Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange ‘, Evance Komu amefungua kinywa chake na kusema; siku mchumba wake huyo atakapotia miguu nchini, wanafunga ndoa.
Masogange kwa sasa (juzi) yupo nchini Afrika Kusini alikokuwa akikabiliwa na kesi ya madawa ya kulevya ambapo alifanikiwa kuwa huru baada ya kulipia faini ya randi 30,000 (shilingi 4,800,000) aliyoamriwa na Mahakama ya Kempton.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni mara baada ya Masogange kuachiwa, Evance alisema anamshukuru Mungu kwa kesi hiyo kumalizika na kinachofuata kwenye uchumba wao ni ndoa tu.
Evance aliweka bayana kuwa kinachomsukuma afanye uamuzi huo kwa sasa ni kutokana na jinsi alivyoguswa na changamoto kubwa alizopitia mchumba wake hivyo ameona kuna kila sababu ya kumuoa kabisa ili apate faraja ya milele.
“Mchumba wangu amepitia majaribu ya kutosha na mimi sioni muda wa kupoteza tena, akitua tu Bongo kinachofuata ni ndoa nina imani itakuwa ndiyo jambo kubwa la kumfariji na kumpa upendo wa hali ya juu,” alisema Evance pasipo kutaja siku ambayo mchumba wake atarejea.
Katika kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili Masogange, alishikiliwa na mwenzake Melisa Edward ambaye naye aliachiwa huru kwa kukosekana na hatia.