kaa tayari kwa blog yangu mpya ya fashion JACK255.BLOGSPOT.COM....

SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG

Monday 27 May 2013

BREAKING NEWS: NEYMAR ATHIBITISHA ANAJIUNGA NA BARCELONA

BARCELONA wamefanikiwa kushinda mbio za kumsaini nyota wa Brazil Neymar kwa ada ya uhamisho ya  £20million kwa mkataba wa miaka mitano.

Mshambuliaji huyo sasa anaelekea barani ulaya baada ya Santos kukubali kumuuza nyota wao waliomng'ang'ania kwa miaka mingi.
Akiandika kwenyepage yake ya Instagram, Neymar alisema: "Nimeongea na marafiki na familia. Jumatatu nitajiunga na Barcelona."
Mabosi wa Barca walienda Sao Paolo kwa mazungumzo mazito kuhusu usajili wa mbrazili huyo, na wakafanikiwa kuwashawishi Santos kumuuza Neymar ambaye angeweza kuondoka bure mwezi Julai.

Neymar alitaka muda kufikiria ofa nyingine kutoka kwa wapinzani wa Barca Real Madrid lakini mwishoni akaamua kwenda Nou Camp.

Kwa usajili huu sasa Neymar atacheza atajiunga na star wa Argentina Lionel Messi na kuunda safu ya ushambuliaji inayotisha barani ulaya.

Neymar ameifungia Santos mabao 138 kwenye mechi 229 tangu mwaka 2009.