kaa tayari kwa blog yangu mpya ya fashion JACK255.BLOGSPOT.COM....

SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG

Sunday 19 May 2013

KIMENUKA IRINGA,MAPAMBANO KATI YA MACHINGA NA POLISI YAMWEKA PABAYA MBUGE MSIGWA SASA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KESHO



Mbunge mchungaji  Peter Msigwa
Polisi  waliotoka  kumkamata  mbunge Msigwa  leo 





 Gari ya  mbunge Msigwa kabla ya  kukamatwa  leo kwa kuhusishwa na vurugu
MASAA  zaidi ya 6 ya mapambano kupiga  mabomu ya machozi na kurushiana  mawe kati ya wafanyabiashara  ndogo  ndogo (machinga ) na  askari  wa  kikosi cha  kutuliza  ghasia (FFU) mkoani Iringa  yaishia pabaya  kwa  jeshi la  polisi kumkamata  mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa  (chadema) na  watu  wengine zaidi ya 60


Polisi  watumia  mabom ya machozi  kutawanya machinga  wapiga mabomu hadi stendi kuu ya mabasi  abiria  walazimika  kutimua  mbinu na kuacha mizigo  yao katika magari   huku machinga  hao wakitumia mawe  na kuchoma mataili  moto barabarani  kuvunja vioo vya gari  la Zimamoto na kuharibu mali mbali mbali kama  njia ya  kupambana na  polisi
Tukio hilo la Mapambano  kati ya machinga na polisi lilitokea leo  kuanzia  muda wa saa 3  asubuhi  na kuendelea  hadi saa 8 mchana katika  eneo la Mashine  tatu  mjini  Iringa na maeneo mbali mbali ya mji  wa Iringa .

Mtandao huu wa na simonbango.blogspot.com ambao ulituma wawakilishi zake  eneo la  tukio  toka  saa 12  za asubuhi  ya jana  alishuhudia kundi kubwa la askari  wa FFU wakiwa na gari la maji ya  kuwasha ambao  wakesha wakilinda  eneo hilo .

Askari  huo  walilazimika  kukesha wakilinda eneo hilo  kufuatia  kauli ya  mbunge  Msigwa aliyoendelea  kuitoa katika  mikutano yake ya hadhara  mjini hapa  kuwhamasisha  machinga  hao ambao  Halmashauri ya Manispa ya  Iringa  iliwahamisha  eneo hilo la mashine tatu  na kuwapeleka  eneo la Mlandege kabla ya  mbunge Msigwa kuwahamasisha  kurejea  tena  eneo hilo.

Kabla ya  mbunge Msigwa  kufika  eneo hilo majira ya  saa 3 asubuhi machinga  hao ambao  walikuwa  wamejikusanya makundi madogo madogo   bila  kupanga  biadhaa zao  walisikika  wakidai  kumsubiri  mbunge Msigwa kama alivyopata  kuwaahidi  kuwa atafika  eneo hilo kuungana nao kwa  kuwa machinga  mpya  .

Hata  hivyo baada  ya mbunge  huyo kufika akiwa na gari lake  la kibunge  ambalo lilikuwa lilikokota tela  la  kuhifadhia mizigo  alisimama  eneo hilo na  kuendeleza msimamo  wake  wa kuwataka machinga  kupambana na baada ya  muda alitoweka  eneo hilo kabla ya  polisi  kuanza  kuwatawanya  machinga hao kwa mabomu ya machozi .

Wakizungumzia  hali hiyo  ambayo ni ya  kwanza kutokea katika  mji  wa Iringa wakazi  wa mji  wa Iringa  walisema  kuwa mbunge  na  viongozi  wengine  wa  serikali  wanapaswa  kulaumiwa kwa  kushindwa  kutumia njia nzuri ya  kukutana  kwa ajili ya kumaliza  mvutano huo  ambao unaendeshwa  kisiasa  zaidi.

Festo Sanga  alisema  kuwa  hali  ilipofikia  ni mbaya zaidi na  hivyo  busara  zinahitajika kwa ajili ya  kutatua  tatizo  hilo  ikiwa ni pamoja na kutazama  eneo zuri kwa ajili ya machinga  bila  kuendelea  kuonyeshana  ubabe .

Sanga  alisema  kuwa machafuko  yaliyojitokeza leo   ni machafuko ambayo wakazi  wa mji  wa Iringa  walikuwa  wakishuhudia katika  vyombo  vya habari  katika  mikoa  mingine  ukiacha  lile la Septemba 2 mwaka  jana lililotokea  kijiji  cha Nyololo kati ya  wafuasi  wa Chadema na polisi na kupelekea kifo cha aliyekuwa mwenyekiti  wa klabu  ya  waandishi  wa habari mkoa  wa Iringa marehemu Daud Mwangosi.

“Kweli katika hili  mbunge wetu hapaswi kuendelea  kulazimisha machinga  kuvunja  sheria  ila anayo nafasi ya  kukutana na viongozi  wenzake  ili  kutafuta  suluhu  ya jambo  hilo vinginevyo wanaoteseka  na machinga na  wale  waliokamatwa kwa  vurugu hizo  ujue  wengi  waliopigwa mabomu ya machozi si machinga  wengine  walikuwa  wasafiri na badhi yao  walikuwa  wakielekea makanisani ”

KUhusu  kukamatwa kwa mbunge  huyo na kuhojiwa na  polisi  juu ya vurugu  hizo Sanga  alisema kwa upande  wake analipongeza  jeshi la  polisi kwa  kutumia busara  zaidi  ya  kumkamata  mbunge   kama mhusika mkuu  na  kuliomba  jeshi la  polisi kuwaachia  wananchi  waliokamatwa  kwa  vurugu  hizo.

Huku  Sarah Kalinga  alidai  kuwa  chanazo cha machafuko hayo ni mvutano kati ya  CCM na Chadema na  kuwa  ilipaswa  vyama vyote  viwili  kukutana na  kuwasaidia  machinga  badala ya  kuwanyanyasa  kwa  kutumia nguvu  kuwabana .

Hata   hivyo  alisema wao kama walalahoi wanampongeza  mbunge wao kwa kuonyesha kuwapigania japo haungi mkono njia  inayotumiwa na mbunge ya  kuwahamasisha   kuvunja  sheria na kuwa  matatizo na majeraha  wanapata  wao  wananchi  na sio mbunge.

Awali  mbunge mchungaji Msigwa  kabla ya  kukamatawa na  jeshi la  polisi alitoweka katika mazingira  tata katika  eneo hilo la mashine  tatu na  kuibukia eneo la chuo  kikuu cha Tumaini Iringa ambako kulikuwa na harambee  ya  kuchangia Kanisa na mgeni  rasmi akiwa  waziri mkuu mstafu Frederick Sumaye na mara  baada ya  shughuli  hiyo  kumalizika ndipo alipokamatwa na polisi na kufikishwa  kituo cha  polisi.

Kabla ya  kukamatwa  kwake mbunge Msigwa alizungumza na mwandishi  wa habari hizi na kuwa  yupo tayari kukamatwa  wakati  wowote na  kuwa kamwe  ataendelea  na msimamo  wake  wa  kuwataka Machinga  kufanya  biashara  eneo hilo.

Mbali ya  kukamatwa  kwa  mbunge  Msigwa  kwa  kuhusishwa na vurugu  hizo pia  jeshi la  polisi  mkoani Iringa  linawashikilia  watu  wengine  zaidi ya 60 akiwemo  aliyekuwa kampeni meneja  wa Chadema  jimbo la Iringa mjini na mgombea  udiwani  kata ya  kwa Kilosa  Abuu Changawa Majeck.

Huku  idadi ya majeruhi  waliojeruhiwa kwa  kupigwa mawe na machinga na  badhi ya machinga  waliokamatwa kwa  vurugu  hizo pia wakijeruhiwa  vibaya  wakati  wakipambana na  polisi hao.

Taarifa  kutoka  jeshi  la polisi zilizothibitishwa na kamanda  wa polisi mkoa  wa Iringa Michael Kamuhanda  zinadai  kuwa  watu  zaidi ya 60 ndio  wamekamatwa  hadi  sasa na  jitihada za  kuwasaka wengine  waliohusika katika  vurugu  hizo ambazo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali  za  wananchi unaendelea.

Huku akidai  mali  mbali mbali  zimeharibiwa likiwemo gari  hilo la zimamoto mjini Iringa pamoja na uharibifu  mwingine  mdogo  mdogo  wa mali za  wananchi .

Jeshi  hilo la polisi  limesema kamwe halipo tayari  kumwachia mbunge Msigwa kwa leo hadi hapo atakapofikishwa mahakamani Kesho