kaa tayari kwa blog yangu mpya ya fashion JACK255.BLOGSPOT.COM....

SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG

Tuesday 24 September 2013

BALOTELLI AFUNGIWA MECHI TATU ITALIA KWA KUMVAGAA REFA .

balo2 0934e
Mario Balotelli akitulizwa na wachezaji wenzake (HM)
balo f48e2
MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amefungiwa mechi tatu kufuata kumvaa refa katika mchezo ambao timu yake, AC Milan ilichapwa mabao 2-1 na Napoli Jumapili.
Balotelli, ambaye alikosa na kufunga bao zuri la kufutia machozi kwa timu yake, alionyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya mechi kwa kumvaa refa.
Mshambuliaji huyo wa Italia sasa atakosa mechi tatu zijazo kwa kosa hilo.
Balotelli, ambaye alifunga penalti zake zote 21 za awali katika mechi rasmi, mkwaju wa Jumapili uliokolewa na kipa wa Napoli, Pepe Reina.
Kadi hiyo nyekundu ya utata, inamaanisha Super Mario atakosa mechi na Bologna, Sampdoria na Juventus, ingawa Milan inaweza kukatia rufaa adhabu hiyo. Chanzo: Binzubeiry

No comments: