kaa tayari kwa blog yangu mpya ya fashion JACK255.BLOGSPOT.COM....

SEARCH FOR ANYTHING IN THIS BLOG

Thursday 3 October 2013

MAJAMBAZI YATEKA BASI LA ABIRIA NA KUPORA SIMU NA FEDHA.



Abiria hamsini na moja waliokuwa wakisafiri na basi la Taqwa kutoka  Bujumbura kuelekea Dar-es-Salaam wametekwa katika kijiji cha Milade wilayani Mkalama na kuporwa mali , simu na fedha zaidi ya shilingi milioni mia mbili hamsini.

Akieleza kamanda wa polisi mkoani Singida bwana Godfrey Kamwela  amesema watekaji hao waliwaamrisha abiria kushuka chini ya basi baada ya kuvunja vyoo na kuanza kuwasachi na kufanikiwa kupora simu, fedha za  kitanzania shilingi milioni tano ,dola za kimaerekani dola laki moja elfu sitini na  faranga zenye thamani ya elfu ishirini kufuatia tukio hilo kamanda Kamwela amewaomba wananchi na makampuni ya simu kushirikiana na jeshi la polisi ili kuweza kuwa kamata watu ambao wamefanya tukio hilo

No comments: